Maafisa wa uokozi katika Jamhuri ya Dominican wanasema watu takriban themanini wamefariki dunia na 150 kujeruhiwa baada ya paa la ukumbi wa burudani kuanguka wakati wa tamasha la msanii Rubby Perez. Msanii huyo ni miongoni mwa hao waliofariki dunia.
Maafisa hao wa uokozi wanawatafuta manusura katika ukumbi huo
ulioko mji mkuu Santo Domingo uliojengwa miaka ya sabini iliyopita.
Mkurugenzi wa Kituo cha Operesheni za Dharura (COE), Juan Manuel Méndez, amesema ana matumaini kwamba wengi wa waliozikwa chini ya paa lililoporomoka bado wako hai.
Jet Set ni klabu ya usiku maarufu huko Santo Domingo ambayo huandaa mara kwa mara matamasha ya muziki wa dansi
Tags
KIMATAIFA