Na Fedrick Mbaruku
Rais wa Jamhuti ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amewaasa wachimbaji wadogo kuachana na vitendo vya utoroshaji wa madini.
Rais Samia ametoa wito huo leo Oktoba 21,2023 wakati akihutubia hafla ya uzinduzi wa mitambo ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo pamoja na mitambo ya shirika la madini la Taifa (STAMICO).
DK.Samia amesema wachimbaji wadogo wanatakiwa kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuhakikisha wanauza madini yao katika viwanda vya ndani kusafisha dhahabu ili kuchochea uchumi wa viwanda.
Pia Rais Samia amewataka wachimbaji kufuata sheria,kanuni na miongozo iliyowekwa katika sekta ya madini ili kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha wananchi na kuchochea maendeleo ya nchi.
Rais Samia amewahakikishia wachimbaji wadogo nchini kwamba serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha mazingira ya uchimbaji pamoja na biashara ya madini ili waweze kuchangia pato la Taifa.
Sanjari na hayo Dk.Samia amesema serikali inampango ambao ni Fira ya 2030 (Vision 2030) unaoelekeza kufanya utafiti wa madini kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya "High Resolution Airborne Graphysical Suvery" ifikapo mwaka 2023.
Aidha kama hatua za mwanzo za utekelezaji wa mpango huo mitambo mitano yenye thamani ya Tsh.Bilioni 2.73 ambayo ikotayari kufanya kazi katika maeneo ya wachimbaji wadogo hapa nchini.