MIKATABA YA UWEKEZAJI WA BANDARI IMEZINGATIA MAONI YA WATANZANIA:DK.SAMIA

Na Fedrick Mbaruku

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassa amesema mikataba ya uwekezaji wa bandari iliyosainiwa imezingatia maoni yaliyotolewa kupitia makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na sheria na kanuni zote za nchi.

Rais Samia ameyasema hayo leo 22 Oktoba 2023 wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba mitatu 3 ya uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam kati ya mamlaka ya Bandari Tanzanja (TPA),Serikali Kampuni ya Dp World ya Dubai iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.

Rais Samia amesema Serikali ilisikiliza maoni mbalimbali yaliyotolewa na chama cha Wanasheria wa Tanganyika,Vyama vya Siasa,Asasi za kiraia,Wanaharakati,Vyombo vya Habari,mitandao ya kijamii,Viongozi wa dini na baadhi ya Viongozi Wastaafu.

Rais Samia amesema mikataba iliyosainiwa imetokana na makubaliano ya awali kati ya serikali na mamlaka ya Dubai ambao wameridhia mahitaji na matakwa ya nchi kama yalivyoainishwa kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

Pia Dk.Samia amesema mikataba iliyosainiwa ni mkataba wa nchi mwenyeji(Host Government Agrement),mkataba wa upangishaji ardhi (Lease Agrement) na mkataba wa uendeshaji Bandari (Conseccion Agrement).

Rais Samia pia amesema uimalishwaji utakaofanywa kupitia uwekezaji huo utakuza biashara ndani na nje pamoja na kuwezesha shughuli za kiuchumi za nchi jirani kuongeza mapato ya serikali na kukuza uchumi wa Taifa.

Aidha Dk.Samia amesema mikataba hiyo imesainiwa kwa kuzingatia kifungu cha sheria namba 6 ya ubia ya mwaka 2023 na kifungu cha 2 cha sheria ya ununuzi wa umma namba 5 yamwaka 2023. 

Previous Post Next Post