BASI LA ALFA LAUA 18 NA KUJERUHI 78


 Na Fedrick Mbaruku

Takribani Watu 18 wamefariki na wengine 78 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha Basi la ALFA na Lori la mafuta baada ya kugongana uso kwa uso na Lori hilo.

Ajali hiyo imetokea mapema leo Oktoba 21,2023 katika eneo la Undomo Kata ya Uchama Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora ambapo chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa Basi hilo kujaribu kulipita lori bila kuchukua tahadhari.

Kwa mjibu wa taarifa zilizotolewa na mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai,kati ya waliofariki 14 ni wanaume na wanne ni wanawake na majeruhi 20 kati ya 78 wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Nkinga kwa ajili ya matibabu.

Aidha zoezi la kutambua miili ya marehemu linaendelea

Previous Post Next Post