SABABU KUONGEZEKA KWA BILI ZA MAJI ZATAJWA

Na Fedrick Mbaruku

WANAFUNZI wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Dodoma wametakiwa kuwa mabarozi katika kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya vyanzo vya nishati husasani katika nishati ya maji na umeme.

Hayo yamesemwa Octoba 4,mwaka huu na Afisa msaidizi Uelimishaji na Huduma kwa wateja kutoka baraza la Ushauri la nishati na maji EWURA CCC Mkoa wa Dodoma Mr.Aman alipofanya ziara yake katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Dodoma.

Amesema suala la kukatika kwa maji ni kutokana na baadhi ya mafundi kuziba mipira ya maji inayovujisha maji na baadae kusahau kurejesha huduma hiyo kwa wananchi.

“Kazi mojawapo ambayo EWURA CCC tunaifanya ni pamoja na kupokea malalamiko yanayofanywa na huduma ya maji,umeme,petrol pamoja na gesi,kuna watu wengine wanamatumizi mabaya ya maji na umeme.

 “Uwa tunawaelimisha wananchi kwamba unaweza ukapata bili kubwa ya maji lakini kumbe mita yako ni mbovu au inawezekana kuna sehemu kunamvujo amabao hauonekani kwa hiyo mwisho wa siku unapata bili kubwa ya maji.

Aidha amewasihi wanafunzi hao kujua na kuwaelimisha wananchi namna ya usomaji wa mita za maji ili kuepukana na ghalama kubwa ambazo zinaweza kujitokeza pindi wanapo taka kulipia bili ya maji ambayo haiendani na matumizi wakati huo. 

Pia amesema matumizi mabaya ya maji ni chanzo mojawapo kinachoweza kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha bili ya maji katika sehemu husika huku akiwataka wananchi kujua matumizi sahihi ya maji kwa kuacha kuosha vyombo na kufua wakati bomba la maji limefunguliwa na maji yanatoka badala yake kufunga bomba mara tu baada ya kukinga maji.

Sanjari na hayo amewashauli wateja wanaotumia nishati ya umeme kuzima taa wakati wa mchana ili kupunguza kiasi cha upotevu wa umeme huku akiwataka kuwashirikisha watoa huduma pindi changamoto zinapojitokeza hali itakayorahisisha upatikanaji wa msaada kwa aliyepata changamoto ya hitrafu ya umeme.      



Previous Post Next Post