DKT.GODWIN AFYA YA AKILI NI HAKI KWA BINADAMU WOTE


 Na Fedrick Mbaruku

NAIBU Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel  amewataka wataalamu wa Afya ya Akili  na makatibu wakuu kutoka sekta ya afya kusimamia teknolojia zinazohitajika katika eneo la matibabu zaidi ili kuweza kuwatibu watu wenye chagangamoto ya afya ya akili.

Kauli hiyo ilitolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani yenye kauli mbiu ya AFYA YA AKILI NI MUHIMU KWA BINADAMU WOTE yaliyoadhimishwa kitaifa Jijini Dodoma katika viwanja vya Nyere Square Octoba 10 mwaka huu.

Alisema upatikanaji wa teknolojia hiyo utasaidia kubaini dalili na kutibu  eneo sahihi kulingana na tatizo la mgonjwa kutokana na wagonjwa wengi hupatiwa matibabu yasiyokidhi tatizo lao 

“Tusimamie kwenye eneo la kujua ni teknolojia gani inayotumika duniani ambayo inahitajika ili tuweze kuwatibu watu wetu kulingana na tatizo.

“Wanaweza wakaonesha dalili zinazofanana lakini sababu zikawa tofauti zilizosababisha hizo dalili,” alisema Dk. Godwin.

Aidha alisema tatizo la afya ya akili ni tatizo la kila mtu katika jamii hivyo aliiomba jamii kwa pamoja kushirikiana katika kuwasaidia wenye changamoto hiyo kwa kuwafikisha katika vituo vya afya ili kupatiwa matibabu ya haraka.

Nae Balozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Milembe Monica alibainisha visababishi vya tatizo la afya ya akili ikiwa ni pamaoja na msongo wa mawazo, matumizi ya madawa za kulevya, matumizi ya pombe kali, kusoma kupitiliza na kusoma kozi nyingi bila kupata kazi pamoja na Baba kuelemea nyumba ndogo.

Hata hivyo Balozi huyo alisema zipo dalili mbalimbali zinazoweza kumpata mtu mwenye tatizo la afya ya akili ikiwa ni pamoja na kuwa mkali kupitiiliza, kutokutunza kumbukumbu,kuongea bila mpangilio,kuanguka kifafa,kuchanganyikiwa,huzuni kila wakati,furaha kupitiliza.

 “Pia yapo madhara yanayoweza kumpata mtu mwenye tatizo la afya ya akili kama vile kuangukia kwenye moto,kuangukia kwenye maji,kuanguka barabarani kwa hiyo tutumieni dawa ili tujikinge na madhara ya afya ya akili,”alisema Balozi Monica

Aidha alisema tatizo hilo linawakumba watu wenye rika mbalimbali huku jinsia ya kike ikionesha kuwa hatalini zaidi kutokana na sababu mbalimbali za kifamilia.

Akitoa takwimu za watu wenye tatizo la afya ya akili Mganga Mkuu wa Serikali Mkoa wa Dodoma Dr.Endlu Methw mwaka 2020/2022 Mkoa wa Dodoma unaonesha kupungua kwa watu wenye tatizo la afya ya akili ambapo mwaka 2020 magonjwa ya akili yalikuwa ni asilimia 35% ambapo yamepungua na kufikia 31.5% kwa mwaka 2022.

Alisema kupungua kwa ugonjwa huo ni kutokana na afua mbali mbali zinazotekelezwa ikiwa ni kuongezeka kwa wataalamu wa afya,vituo vya afya na utoaji wa elimu kwa jamii.

Alisema hadi sasa Mkoa wa Dodoma unakabiliwa na ugojwa wa kifafa ambao kati ya wagonjwa wa afya ya akili kwa mwaka 2022 walikuwa 24,183 huku idadi ya watu wenye kifafa ikiwa ni 19 sawa na 79%. 

Ailisema bado kuna changamoto mbalimbali hasa uwezo wa kiuchumi kuwa duni kwa wagonjwa wanao athirika na afya ya akili hali inayowafanya wahanga wengi kushindwa nkufika katika vituo vya kutolea huduma hiyo.

“Wengi wanakuwa hawana uwezo wa kumudu ghalama za matibabu kutokabna na ghalama kuwa kubwa na hivyo wanakuja kufika kwetu kwa kuchelewa.

Previous Post Next Post