WAKAZI WA MKOA WA DODOMA NA MAENEO YA JIRANI WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA MAPOKEZI YA MWENGE

 

Na Fedrick Mbaruku

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe.Jabir Shekimweli ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani kujitoleza kushiriki katika mapokezi ya Mwenge wa uhuru unaotarajia kuwasili Oktoba 3,mwaka huu Mkoani humo.

Mhe.Shekimweli ameyasema hayo leo oktoba 2,mwaka huu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mapokezi ya Mwenge wa uhuru utakaopokelewa na kuanza kukimbizwa kutoka eneo la Veyula saa 12 asubuhi Oktoba 3,mwaka huu katika Wilaya ya Dodoma Mjini.

Amesema Mwenge unatarajia kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo na kushiriki kutoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru.

“Nichukue nafasi hii kwa niaba ya Viongozi kwenye Wilaya,wapenda maendeleo wote na wadau wakubwa wa mwenge wa uhuru wanao enzi tunu ya Taifa kuwaalika mshiriki tangia katika mapokezi ya mwenge wa uhuru.

Pia ameyabainisha maeneo ambayo mwenge utatembelea ikiwemo eneo la Chuo cha Mipango,Hombolo,Kampasi mpya ya Miyuji,Ilazo,Mradi wa Barabara ya Nzuguni yenye urefu wa Km 5,Mradi wa maji Nzuguni ulioghalimu Tsh.Bilioni 4.8,kituo cha afya cha Nkuhungu Mnada mpya na Nala pamoja na kutembelea kikundi cha vijana walioanzisha kiwanda cha thamani ya ngozi (Faru Product). 

Pamoja na hayo amesema mwenge utakagua klabu za wapinga rushwa na madawa ya kulevya katika eneo la Chuo cha Veta.

Aidha ameongeza kuwa wakati wananchi wakiendelea na sherehi hizo za mwenge wa uhuru kutakuwepo pia wasanii mbalimbali watakao toa burudani katika mkesha huo.

Previous Post Next Post