Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini kutumia kwa weledi vifaa tiba na kutunza magari ya wagonjwa ili kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa Wananchi.
Dk.Samia ameyasema hayo leo 28,Oktoba,2023 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya mareria Tanzania ya mwaka 2022 na ugawaji wa magari ya wagonjwa na vifaa tiba iliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es salaam.
"Tununue vifaa viende huko vikawasaidie watu ngazi ya chini na vifaa hivi ni vya kisasa hata uende marekani leo watakupima na hivihivi tunaomba mkavitunze vikatunzwe vitowe huduma kwa watu wengi,"Dk.Samia