Na Fedrick Mbaruku
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philp Mpango amesema katika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi yam waka 2020 serikali imedhamilia kuendeleza sekta ya kilimo,sekta ya mifugo na uvuvi ili kuongeza uzalishaji tija na thamani ya mazao ya kilimo,mifugo na uvuvi pamoja na kukuza kipato na kutoa ajira kwa wananchi.
Dk.Mpango ameyasema hayo Agosti,01,mwaka huu alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya sherehe za wakulima (Nanenane) yaliyofanyika katika viwanja vya Jijini Mbeya.
Dk.Mpango amesema serikali imeongeza bajeti ya wizara ya mifugo na uvuvi kutoka kiasi cha shilingi Bilioni 275 mwaka 2021/2022 hadi shilingi Bilioni 295 mwaka 2023/2024 huku bajeti ya wizara ya kilimo ikiongezeka kutoka shilingi Bilioni 294 mwaka 2021/2022 hadi kufikia shilingi Bilioni 970.78 mwaka 2023/2024 ambalo ni ongezeko la asilimia 330.
Dk.Mpango amesema ongezeko hilo linalenga kuimalisha maeneo ya utafiti na huduma za ugani,kutoa luzuku za pembejeo za kilimo mifugo na uvuvi,kuimarisha na kutoa huduma ya upimaji wa afya ya udongo,kuendeleza kilimo cha umwagiliaji,kuimarisha upatikanaji wa mitaji ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfuko wa maendeleo ya kielimu,kuimarisha miundombinu ya hifadhi ya mazao ya kilimo,kuhamasisha na kuanzisha kilimo cha mashamba makubwa ya pamoja na kuimarisha maendeleo ya ushirika.
“Mauzo ya mazao ya chakula yamekuwa chanzo cha kuongezeka kwa mapato ya uchumi wa nchi yetu kwa mfano thamani ya mauzo ya mazao nje ya nchi yameongezeka kutoka dola Milioni 57,97,279 mwaka 2021 hadi kufikia dola za kimarekani Milioni 71,543,641 mwaka 2022 thamani ya mauzo ya ufuta yameongezeka kutoka dola Milioni 123627 mwaka 2021 hadi kufikia dola Milioni 143,788,838 mwaka 2022.
“kwahiyo napenda kutoa rai kwa wakulima nchini kote kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula ili nchi yetu ijitosheleze kwa chakula na kupata fedha Zaidi kutokana na uzalishaji wa mazao mbalimbali,”Dk.Mpango
Aidha Dk.Mpango amesema katika kuongeza matumizi ya mbolea nchini serikali inaendelea kuimarisha upatikanaji na kuhimiza matumizi ya mbolea kupitia mpango wa luzuku ili kuongeza tija na uzalishaji huku akisema kupitia mpango huo matumizi yam waka 2022/2023 yamefikia tani 5,80,628 ikilinganishwa na tani 3,63,599 mwaka 2021/2022 .
Pia amesema kwa kutambua umuhimu wa vijana kunaumuhimu wa kuongeza fursa za ajira na kusema wizara ya kilimo imeanzisha mradi wa BBT (Building a Better tomoorow) ambao hadi sasa umetoa vituo atamizi 13 ambapo vijana 812 ambao kati yao wanawake ni 282 wakati idadi ya wanaume ikiwa ni 530.
Makamu wa Rais amesema lengo la kuanzishwa kwa miradi hiyo ni kuwawezesha vijana kupata uzoefu katika kuanzisha na kuendesha miradi ya kilimo,ufugaji na uvuvi kibiashara pamoja kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa mazao bora kwa ajiri ya mifugo,marighafi za viwanda na kuongeza fursa za ajira.