Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Stegomena Tax amesema serikali itaendela kukihifadhi chumba maalumu cha Mahakama ya Kimataifa Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ambacho kilitumika kuendesha kesi za mauaji hayo yam waka 1994 kilichopo katika jengo la kituo cha mikutano cha kimataifa Arusha (AICC) Jijini Arusha.
Waziri Tax ameyasema hayo hii leo 10, Agosti,mwaka huu wakati wa ziara yake ya kukagua vitegauchumi vinavyosimamiwa na kituo jijini Arusha ikiwemo ya kumbi za mikutano,Hospitali,nyumba za makazi pamoja na kiwanja kikubwa ambacho panajengwa kituo kikubwa cha mikutano cha Kilimanjaro International Convention Cerntre.
Akiwa ziarani Dkt.Tax amesema lengo ni kukuza diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na mataifa mengine duniani ambapo waziri Stegomena anakagua taasisi ya mikutano ya kimataifa ya AICC iliyopo chini ya wizara yake