Fedrick Mbaruku
Watu wawili wameuawa na wengine saba kujeruhiwa katika shambulio Dhahiri la kombora la Urusi katika mji wa Zaporizhia nchini Ukraine,kwa mjibu wa maafisa wa Ukraine Video iliyotumwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ilionesha moshi ukifuka kutokana na kuungua na kuharibiwa vibaya kwa majengo karibu na kanisa.
Hayo yamejiri mapema leo 10, Agosti,mwaka huu nchini humo ambapo katika Donetsk inayodhibitiwa na Urusi mashariki mwa Ukraine,mtoto aliuawa na watu wawili kujeruhiwa wakati kombora la mizinga la Ukraine lilipopiga jengo la Ghprofa mbili.
Kwa mjibu wa Wizara ya ulinzi nchini Urusi imesema kuwa vikosi vyake vilidungua ndege mbili zisizo na rubani za Ukraine karibu na mji mkuu wa Moscow ambapo moja iliangukwa karibu naa wilaya ya kusini ya viwanja vya ndege vikubwa vya kimataifa vya Urusi na nyingine karibu na barabara ya Minsk.
Sanjari na hayo maafisa nchini humo wameripoi mlipuko kwenye uwanja wa kiwanda kinachotengeneza vifaa vya macho vya vikosi vya usalama vya Urusi kaskazini mwa Moscow.
Aidha maafisa hao hawajatoa sababu zinazoshukiwa za mlipuko huo ulioua mtu mmoja na kujeruhi wengine 60 na kuwaacha takribani watu wanane kusikojulikana.