Na Fedrick Mbaruku
Katika mchezo wa Ngao ya Jamii Timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC imetoka sale dhidi ya Singida Fontein Gati mchezo ambao umepigwa katika uwanja wa mkwakwani Mkoani Tanga.
Mchezo huo umechezwa leo 10, Agosti,2023 ambapo Timu hizo zimetoka bila bila katika kipindi cha kwanza na katika kipindi cha pili.
Kwa mjibu wa sharia za soka Timu hizo zimechuana kwa mikwaju ya penati akianza na Azizi Andambwile aliyekosa penati ya kwanza wakati penati ya kwanza kwa simba alifumua Luiss Miquison na kuipa Simba ushindi wa bao la kwanza.
Penati ya pili imepigwa na Maluu chakei aliyeipa ushindi wa bao la kwanza kwa singida wakati Saidontibazonkiza akipiga mkwaju wa penati na kuipa bao la pili simba huku yusufu kagoma akikosa penati ya tatu na penati ya tatu upande wa simba ikipigwa na Mzamilu Yasin akipiga goli la nne,waka Duke akipiga Penati ya tano kwa singida,Simba ikimalizia na Moses Phili.
Mchezo huo umemalizika kwa mikwaju ya Penati ambapo Simba wameibuka na ushindi wa magori 4 wakati singida wakitoka na mabao 2 na kuipa nafasi Simba SC ya kunyukana na Yanga FC jumapili 13,Agosti,2023 katika Dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es lamaa.