MIKOPO YA ASILIMIA NNE KUREJESHWA KIVINGINE

Na Fedrick Mbaruku
Naibu Waziri wa Tamisemi Deogratias Ndejembi amesema serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele katika kuhakikisha inawawezesha vijana katika nyanja tofauti ili kukuza thamani ya mnyororo wa upatikanaji wa fursa za ajira.
Mhe.Ndejembi ameyasema hayo 07,Agosti mwaka huu wakati wa ufunguzi wa kingamano la vijana lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete uliopo Jijini Dodoma.
Mhe.Ndejembi amesema vijana wengi nchini wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa mitaji kutokana na ugumu wa kukopesheka wanapoenda katika taasisi mbalimbali za kifedha na kusema serikali imeweka mipango Madhubuti ya kuhakikisha vijana wanapata mitaji itakayowasaidia kuanzisha na kuendesha shughuli zao za kimaendeleo.
Pamoja na hayo Ndejembi amesema serikali inaendelea kufanya mapitio ya mikopo ya asilimia nne iliyozuiliwa kwa muda mara tu baada ya kutolewa kibari na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mikopo hiyo ilitaendelea kutolewa kama ilivyokusudiwa ili kuleta mwanya wa upatikanaji wa ajira kwa vijana.
Amesema matarajio ya serikali ni kutaka kuona vijana mbalimbali nchi wenye mawazo yanayoweza kuongeza tija na ufanisi katika Taifa waweze kupewa mikopo ya asilimia kumi na kusema silazima awe ni mwanakikundi au awe na wanakikundi wenzake.
Amesema baada ya mchakato kukamilika kutakuwa na mabadiliko katika utoaji wa mikopo hiyo.
Hata hivyo Ndejembi amesema moja kati ya changamoto inayotazamwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ni pamoja na namna ya vijana kupata taarifa ya mikopo huku akiwahakikishia vinana mkoani humo kuwa serikali inadhamira njema kwa vijana wote nchini.
Nae Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara Ndugu Anamlingi Macha amesema amewataka vijana mkoni humo kulitumia kongamano hilo kama fursa adhimu ili kuendana na ilani ya chama cha mapinduzi hususani katika kutekeleza suala la ajira kwa vijana

Previous Post Next Post