MAAGIZO MATANO YA MAKAMU WA RAIS KWA HALMASHAURI ZOTE NHINI

Na Fedrick Mbaruku

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philp Mpango amewataka vijana Mkoani Dodoma na Mikoa mingine kutambua fursa zitakazowawezesha vijana kujipatia maendeleo ya kiuchumi na taifa kwa ujumla. 

Dk.Mpango ameyasema hay oleo wakiti akifungua kongamano la vijana Mkoani humo lililofanyika 07,Agosti katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Dk.Mpango amesema lengo la kongamano hilo ni kutaka kuwawezesha vijana mkoani humo,kujadili utekelezaji wa sera na miongozo mbalimbali na jinsi inavyowanufaisha vijana.

Amesema uendelezaji na ushirikishwaji wa vijana ni ajenda mhimu katika kujenga na kukuza uchumi na kusema ushiriki wa vijana katika uwekezaji ni jitihada ambazo zinapaswa kuungwa mkono na kutekelezwa kwa vitendo.

Mhe.Makamu wa Rais amesema kwa kutambua umuhimu wa vijana na kwakuongeza fursa za ajira serikali imebuni na kutekeleza program mahususi ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili kupitia mpango wa jenga kesho iliyo bora (Building a Better Tomoorow) BBT, ambao unalenga kshiriki kwa vijana katika sekta ya kilimo kwa kuwapatia elimu,mashamba,mitaji na kuwaunganisha na fursa za masoko.

Amesema katika program hiyo hadi sasa kuna vituo atamizi 13 ambapo vijana 812 ambao kati yao ni 282 na wanaume ni 530 wameanza kupatiwa mafunzo ya kilimo cha mazao ya kibiashara huku akisema katika sekta ya mifugo na uvuvi inajumla ya viatamizi 8 vyenye jumla ya vijana 238 ambao kati yao wanawake ni 71 na wanaume ni 167 ambao wanaendelea na mafunzi ya kunenepesha mifugo.

Hata hivyo Dk.Mpango amesema lengo la vituo hivyo ni kuwawezesha vijana kupata uzoefu katika kuanzisha na kuendesha miradi ya kilimo,ufugaji na uvuvi pamoja na kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa mazao bora ya mifugo,malighafi za viwanda na kuongeza fursa za kujiajiri.

Aidha Dk.Mpango amesema serikali inaendelea kutoa mafunzo atamizi ya uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji kwa vijana kwa kushirikiana na asasi za kiraia ambapo hadi sasa wapo vijana 200  ambao kati yao 70 ni wanawake na 126 ni wanaume huku akisema mpango wa serikali ni kuendelea kutoa mafunzo kwa vijana ni 750.

Dk.Mpango amewasihii vijana mkoani humo na mikoa mingine kuchangamkia fursa ili kujipatia ajira na kukuza uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Dk.Mpango ametoa rai kwa vijana nchini kote kujitokeza na kushiriki katika juhudi za kukabiliana na uhsribifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuhakikisha maendeleo yanakuwa endelevu nchini.

“Naomba muongeze nguvu kwenye masuala ya uhifazi wa mazingira kwa kupanda miti kupendezesha mji wa Dodoma na maeneo mengine nchini kuhakikisha usafi wa mazingira katika maeneo yetu na sehemu za kufanyia biashara,lakini fursa nyingine za ajira zinazo endana na mazingira ni pamoja na kuanzisha na kuendesha kampuni za ukusanyaji wa taka,uzalishaji wa funza zinazotokana na taka kwa ajiri ya chakula cha kuku na samaki,biashara ya hewa ya ukaa,uanzishaji wa vital una kufanya biashara ya miche ya miti laikini pia ufugaji wa nyuki na kadhalika.

“Napenda niwaahidi kwamba serikali ya chama cha mapinduzi itafanyia kazi changamotomoto zote nilizozisikia ikiwemo changamoto kubwa ambayo ni mitaji lakini pia ukosefu wa maeneo ya kufanyia kazi ,utaalamu n ahata mashine kwahiyo tutashirikiana na sekta mbalimbali kama mabenk na nyingene kama sido,”Dk.Mpango

Pia amesema ili kuimalisha na kuendeleza juhudi za serikali katika kuinua ushiriki wa vijana katika uzalishaji Halmashauri zote nchini zihakikishe zinawaunganisha vijana katika uzalishaji ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za taasisi za kifedha zitakazo tumika kupembua changamoto zao hususani upatikanaji wa mitaji,Halmashauri zItenge maeneo maalumu kwa ajili ya uzalishaji mali kwa vijanaikiwemo kuanzisha kongani zinazoendana na fursa zilizopo katika maeneo yao,kuwaunganisha vijana na fursa za uwekezaji kama vile pembejeo za kilimo mfuko wa maendeleo ya wanawake mfuko wa maendeleo ya vijana pamoja na program za mikopo katika benki,Halmashauli zihakikishe zinatengeneza kanzi data ya vijana na ujuzi pamoja na taaluma zao ili kuweza kuwaunganisha na fursa mbalimbali zinazojitokeza,Halmashauri zihakikishe zinawahamasisha vijana katika kuunda Clab za mazingira katika shule,Vyuo na taasisi nyingine ili ziwezekuchangia shughuli za uhifadhi wa mazingira. 

Katika suala la maadili Makamu wa Rais amesema baadhi ya vijana walio wengi hususani mijini yamepolomoka kutokana na vijana kujihusisha na vitendo visivyofaa kwa kukosa uaminifu,kukosa utii wa sharia,kutokuitii serikali,bidi ya kazi ni ndogo,tamaa ya kupata fedha haraka haraka kwa njia zisizo kuwa za kihalali na kutokuwajibika kwa uma kwahiyo hili ni tatizo ambalo matokeo yake ni mabaya kamahalitashughulikiwa ipasavyo.

“Uadilifu ni sifa kuu ya kila mwananchi maana vijana wakikosa uadilifu tutapata wapi viongozi wa kesho kwa hiyo wito wangu kwa vijana wote katika taifa letu nawaomba sana jiepusheni na matendo yote yasiyoendana na maadili yetu kwa mfano matumizi ya dawa za kulevya,unyang’anyi,mapenzi ya jinsia moja rushwa pamoja na utapeli mukumbuke kwamba uadilifu ni mtaji wa kuaminika na kufanikiwa,”Dk.Mpango

Previous Post Next Post