Na Fedrick Mbaruku
Waziri wa kilimo Mhe.Hussen Bashe amewataka wananchi Mkoani Mbeya kuacha kuvamia katika ameneo yaliyotengwa kwa ajili ya utafiti na kusema serikali hatasita kuwaondoa watakao bainika kuvamia katika mashamba ya mbegu.
Mhe.Bashe ameyasema hayo leo 8, Agosti,mwaka huu wakati wa kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane yaliyofanyika katika uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya
Mhe.Bashe amesema kutokana na ujenzi wa barabara nne ameomba kujengwa kwa daraja la juu kati ya Tariuyole utakao ingia katika uwanja wa ndege kimataifa ili kurahisisha mwingiliano wa watu katika eneo hilo.
“Nataka niwahakikishie wakulima mama amefungua pochi nendeni mkalime mutauza mazao ambayo itawafanya wafnyabiashara ambao walikuwa wananunua mahindi kwa shilingi miambili sasa wanunue kwa bei halisi,”Mhe.Bashe
Mhe.Bashe ameitaja mikoa inayofanya vizuri katika sekta ya kilimo cha mazao ya nafaka ambayo imekabidhiwa tuzo ukiwemo mkoa wa Ruvuma,Rukwa,Mbeya na katika mikoa ambayo anaongoza kwa kilimo cha mazao yasiyokuwa ya nafaka ni pamoja na Kagera,Kigoma na Mbeya.
Pia ametoa wito kwa wakulima kuwekeza na jikita katika kilimo cha kisasa huku akisema serikali imepanga kuwekeza katika sekta ya kilimo hasa katika kutatua changamoto za wakulima nchini.