WAZIRI KAIRUKI AHIMIZA UFANISI,UWELEDI,UWAJIBIKAJI NA UTOAJI HUDUMA BORA SEKTA YA ELIMU NCHINI AWATAKA MAAFISA ELUMU SEKONDARI KUONDOA VISINGIZIO

Na Fedrick Mbaruku

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Angellah Kairuki amewataka Maafisa Elimu Sekondari wa halmashauri zote nchini kuongeza kasi katika utendaji kazi na kujitathimini ili kuhakikisha wanapiga hatua na kasi katika maendeleo na usimamizi wa sekta ya elimu ya sekondari.

Waziri Kairuki ameyasema hayo leo julai 5,mwaka huu wakati wa hafla ya kukabidhi magari 51 kwa maafisa elimu hao iliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Dodoma.

Mhe.Kairuki amesema maafisa elimu wanatakiwa kujifunza kutokana na matokeo yanayopatikana na kutafuta mbinu mbalimbali za kutatua changamoto pale zinapojitokeza pamoja na kuwa na usimamizi mzuri ili kuleta mafanikio bora katika sekta ya elimu.

Waziri Kairuki amesema kwa kutambua jukumu la usimamizi wa elimu ya sekondari na kusema linahitaji uwajibikaji na usimamizi thabiti na usimamizi wa hali ya juu katika ngazi ya Taifa,mikoa,wilaya,halmashauri,kata na sehemu husika huku akisema mafanikio katika usimamizi wa elimu pamoja na bidii,ufanisi,tija,uweledi,ubunifu,uaminifu na utiifu bado yanategemea uwezeshwaji wa vifaa na vitendea kazi kwa wasimamizi husika. 

“Nilikuwa naongea na makatibu tawala wasaidizi wa TSC na maafisa utumishi wanaoshughulikia mfumo wa human capital management information system niliwakumbusha tu wakumbuke kwamba walimu wetu katika halmashauri ni zaidi ya asilimia 50 au zaidi ya idadi yote ya watumishi wa umma waliopo katika taifa letu.
“Kwahiyo na nyinyi naendelea kuwakumbusha kwamba maafisa elimu wa sekondari mkumbuke kuwa tunasimamia kundi kubwa,kundi la muhimu na sikwamba makundi mengine siyamhimu lakini kwa idadi yake wapo wengi najua mmekuwa mkifanya kazi nzuri kwahiyo tuendelee kuona ni kwanamna gani tutaweza kusimamia vyema sekta hii.

"Lakini pia tutafute njia ya kuona namna gani tutaweza kuwasimamia walimu wetu vizuri,kuendelea kuangalia usitawi wao,kuhakikisha kiwango kinachotolewa katika stad za kujifunza na kujifunzia zinakuwa ni zile kama ambavyo tunaendelea kupewa kutoka kwa wataalamu wetu wa mitaala na maelekezo mbalimbali,”amesema Mhe.Kairuku

Pia amesema magari hayo ni ya awam ya nne ya ununuzi na sehemu ya ugawaji kwa maafisa elimu wa sekondari ambapo katika awamu tatu zilizotangulia takribani magari 95 yalipokelewa na magari 89 yalipokelewa katika ngazi ya halmashauri wakati magari manne yalipokewa katika ngazi ya wizara na gari moja likipokelewa kwa ajiri ya shirika la elimu la kibaha.

Amesema hatua hiyo ni mwendelezo wa juhudu za serikali ya awamu ya sita katika kuendelea kuboresha sekta ya elimu na kusema serikali inamatarajio kuwa magari hayo yaliyogawiwa leo yatakuwa ni nyenzo muhimu kwa maafisa elimu sekondari katika halmashauri zote nchini ili kuweza kufuatilia vyema na kusimamia utoaji wa huduma ya elimu nchini.

Hata hivyo Waziri Kairuki ameitaka mamlaka husika kuyatengea fedha kwa ajili ya bajeti ya uendeshaji wa magari hayo pamoja na matengenezo pale yatakapokuwa yamehitajika ili yatumike vizuri na kudumu kwa muda mrefu na kuleta ufanisi na ubora wa elimu katika utekelezaji wa majukumu ya sekondari katika ngazi za halmashauri.
“Tunaamini hakutakuwa na visingizio ya ninyi sasa kutokuwa na nafasi ya kuweza kutembelea na kukagua shule zetu kuweza pia kufika katika shule zetu ili kuweza kuwasikiliza walimu na wasimamizi wengine wa sekta ya elimu kuanzia kata mpaka juu lakini pia kuweza kufuatilia maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu badala ya kuwasubili walimu na watumishi wengine katika sekta hiyo kufuata huduma.

Waziri Kairuki ametoa rai kwa maafisa hao kusimamia matumizi sahihi ya magari hayo na kutenga bajeti za mafuta pamoja na matengenezo ili yaweze kufanya kazi kama ilivyokusudiwa huku akisema serikali inayafanya hayo ikiwa ni utekelezaji wa liana ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020 hususani ibara ya 78 inayoelezea huduma za jamii upande wa elimu.

Pamoja na hayo amewataka pia kusimamia ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na sekondari unaoendelea nchini.    

Previous Post Next Post