MKE AMUUA MME WAKE KWA KUMKATA NA SHOKA KICHWANI

Na Fedrick Mbaruku

Mwanamke mmoja alinaefahamika kwa jina la Anastela Manyika na mkazi wa Kijiji cha Kisumba Kata ya Matanga Mkoani Rukwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mme wake Vitus Kisi (50) kwa kumkata na shoka kichwani.

Akizungumza na Maulus Media kwa njia ya simu Mwenyekiti wa Kijiji hicho Filbert Seleu leo Julai 8 mwaka huu amesema chanzo cha kifo hicho ni mme wa mke aliyetekeleza mauaji hayo kudai mke wake anatumia vibaya fedha alizokuwa ameziifadhi.

Seleu amesema baada ya mwanamke huyo kumjeruhi mme wake alikimbilia na baada ya kusakwa alikutwa kajificha kwa Dada yake,mtoto wake alimuwahisha hospitalini wakiwa njiani ndipo umauti ulimkuta huku akibainisha kuwa marehemu amefariki akiwa na familia ya watoto saba.

“Baada ya kupokea taarifa na muuguzi wa zahanati ya Kisumba akinitaarifu kuwa Vitus Kisi amejeruhiwa na Mke wake mtoto wake amemleta kutibiwa na hili jeraha haliwezekani kutibiwa hapa mpelekeni hospitali ya Mkoa kwa ajili ya matibabu  moja kwa moja nikaenda kumuona basi walivyokuwa wanampekeleka kutibiwa kufika kijiji cha matanga akawa amekata roho na kurudisha mwili wa marehemu.

“Nilivyowapigia polisi simu walikuja kwa haraka na kufanya uchunguzi na kuruhusu mwili wa marehemu uzikwe kasha wakamchukua mutuhumiwa wakaondoka nae hivi yupo mahabusu,”Amesema Seleu 

Previous Post Next Post