WAKAZI WA MKOA WA DODOMA WATAKIWA KUJITOKEZA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JKT

Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani kujitokeza katika maonesho ya jeshi la kujenga Taifa (JKT) yanayoendelea katika viwanja vya Jengo la SUMA JKT Medali Mashariki ikiwa ni siku chache kuanza wiki ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanza kwake..

Mhe.Senyemule ametoa rai hiyo leo julai 4,2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Jengo la Mkapa Jijini Dodoma. 

Mhe. Senyamule amesema kuwa Maonyesho hayo  yameanza  Julai 1 hadi 9 ndio itakuwa ni kilele chake na yanatarajiwa  kufanyika katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.

"Niko hapa kutoa rai kwa wakazi wa Dodoma na watanzania wa mikoa ya jirani kutenga muda wao kutembelea maonesho hayo kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yaliyofanywa na Jeshi letu,”amesema Mhe. Senyamule

Pia Mhe.Senyemle amesema katika maonyesho hayo kuna teknolojia mbalimbali kuhusu masuala ya kilimo, uvuvi, useremala na kadha wa kadha.

Aidha, Mhe. Senyamule ametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki maonyesho hayo ili kupata fursa mbalimbali zilizopo katika maonyesho hayo. 

"Ni fursa kubwa sana kwa jamii  hususan vijana kutembelea eneo hilo la maonesho kwa lengo la kujifunza namna ya kujiajiri kwa kutumia fursa zilizopo hapa nchini" amebainisha Mhe. Senyamule 

Hata hivyo,ameendelea kutoa wito kwa wananchi wote kwa ujumla wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi siku ya kilele ya maadhimisho hayo katika  Viwanja vya Jamhuri na kusisitiza kuwa viwanja vitakuwa wazi kuanzia saa 12 asubuhi.

Previous Post Next Post