Na Samwel Erastus
Dakika 120 zimeweza kuamua ubingwa wa fainali ya ligi ya vijana chini ya miaka 20 na Mtibwa Sugar kufanikiwa kutetea ubingwa mara ya tano hii leo dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Fainali hiyo ulimalizika kwa ushindi wa bao 1~0 Athuman Makambo akaifungia Mtibwa bao lake la saba na kuibuka kinara wa mabao ligi ya vijana chini ya miaka 20.
Mtibwa sugar imeruhusu mabao mawili tu katika msimu huu kwenye michuano hiyo ambayo imetamatika hii leo.
Geita gold fc imeshika nafasi ya pili, Azam fc imemaliza ya tatu na kagera sugar fc ikimaliza nafasi ya nne.
Tags
MICHEZO