RAIS DK.SAMIA AHITIMISHA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUPAMBANA NA RUSHWA BARANI AFRIKA AWATAKA CAG,DPP NA WENGINE WAKASOME

Na Fedrick Mbaruku

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa inafanya kazi kwa weledi na ufanisi ili kukabiliana katika kupinga na kutokomeza vitendo vya Rushwa nchini.

Rais Dk.Samia ameyasema hayo leo 11 julai,2023 katika kilele cha maadhimisho ya siku ya kupambana na Rushwa barani Afrika na miaka 20 ya utekelezaji wa mkataba wa umoja wa Afrika wa kuzuia na kupambana na rushwa yaliyofanyika Mkoani Arusha.

Rais Dk.Samia amesema moja kati ya vikwazo vikubwa vya maendeleo barani Afrika ni pamoja na janga la rushwa suala linalotajwa kuzoofisha mifumo ya kitaasisi na kuathili mipango mikakati ya kujikomboa kiuchumi na kusema vindo vya rushwa haviishii katika mipaka ya Taifa bali ni miongoni mwa makosa yanayovuka mipaka ya Taifa.

“Nilikuwa nafuatilia mkutano huu tangu ulipoanza nilikuwa nafuatilia kwenye tv nikipata nafasi nikiona mijadala na nimesikia taasisi mbalimbali,watu mbalimbali,watoa mada mbalimbali wakijadili rushwa katika maeneo kadhaa wapo waliosemwa sana kwenye mkutano huu ambao ni sisi wanasiasa ambao tunaendekeza sana rushwa.

“Lakini pia wamezungumzwa wafanyabiashara,kwa bahati mbaya vyombo vya ulinzi na usalama jeshi la polisi,maofisini tunakofanya kazi nako wamelaumiwa halikadhalika mahakamani nako hakukunusulika vilevile na vyuo vya juu na wote tuliohudhulia hapa tumeona kwa takwimu na nilikuwa naona picha zikioneshwa kwa ushahidi kuonesha rukwa ilivyoshamili katika maeneo hayo,”amesema Dk.Samia

Amesema kwa wale wote waliohusika na vitendo hivyo sekali itafatilia maadhimio ya mkutano huo ili kufanya malekebisho katika maeneo hayo huku akiwapongeza watu na mashirika ya kiserikali na yasiyokuwa ya kisekari kwa kazi mbalimbali wanazozifanya katika kuzuia na kupambana na rushwa.

Dk.Samia amesema Viongozi wa umoja wa Afrika waliamua kufanya mkataba huo ambao hadi sasa umitimiza mika 20 katika utekelezaji wake ambao ni mfumo wa kisheria unaoziwezesha nchi za afrika katika kushirikiana katika kuzuia na kupambana na Rushwa pamoja na kuwachunguza watuhumiwa wa makosa na urejeshwaji wa mali zilizotokana na vitendo vya Rushwa.

Amesema mkataba huo umeweka misingi ya kisheria ya nchi za Afrika kushirikiana katika mafunzo ya kiweledi yanayohusu na namna ya kuzuia na kupambana na Rushwa,kupeana msaada wa kisheria pamoja na ushirikiano wa kiufundi katika kushughulikia kwa haraka maombi ya vyombo vilivyopewa jukumu la kuzuia,kuchambua,kuchunguza na kuadhibu washitakiwa wa makosa ya Rushwa.

Dk.Samia amesema maadhimisho hayo ni nyenzo muhimu itakayowezesha kutafakari kwa kina kwa uwazi na kwa dhati kuhusu utekelezaji wa mkataba wa umoja wa Afrika wa kuzuia na kupambana na Rushwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Hatahivyo Dk.Samia amewataka watanzania wote kutafakari na kutathimini matarajio ni yapi baada ya mkataba huo ili kuweza kuidhibiti Rushwa na kuendana na kaulimbiu ya mwaka huu.

Pia Dk.Samia amesema Tanzania ilisaini mkataba huo 5 Novemba 2003 na kulidhia 22 Februari 2005 ambapo ulianza kutumika rasmi 5 Agosti 2006 na kusema Tanzania ni miongoni mwa nchi 48 kati ya nchi 55 zinazosaini na kulidhia mkataba huo.

Katika hatua nyingine Rais Samia amesema Tanzania inamakubaliano na nchi mojamoja na ni mwanachama wa jumuia na mashirika ya kikanda na kimataifa ya kuzuia na kupambana na Rushwa.

Dk.Samia amesema serikali imeongeza uwazi katika shughuli za serikali na kusema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali itaendelea kufanya vizuri katika sekta za umma na kuongeza uwazi ili kuimalisha mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa nchini. 

“Swali tunalipaswa kujiuliza waafrika wote ni kwamba Je,kila mmoja wetu kwa nafasi yake amefanya vya kutosha kutimiza wajibu wakewa kuzuia na kupambana na Rushwa ? nilimsikia Waziri Halun kutoka Zanzibar akisema anawaombea vijana wanaofanya kazi kwenye taasisi za kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wapelekwe maeneo yenye ufanisi mkubwa wakajifunze imekuwaje mpaka wale wamefanikiwa.

“Nikamwambia sio vijana tu lakini linapaswa kuanza na sisi kwa hiyo kama tunaweza tukapeana na sisi watono watano nendeni kasomeni imekuwaje tunaweza tukafanya kitu kama hiki kwa sababu kama ilivyosemwa kwa kiasi kikubwa wanasiasa tunahusika sana kwenye jambo hili kwa hiyo wanasiasa twendeni tukasome alafu tukirudi vyombo vyetu sasa wakina CAG,DPP, MAADILI na wenyewe nao waende wakasome vimefanya vipi mpaka imewezesha hivyo alafu sasa wanakuja watumishi wetu wa TKUKURU,”amesema Dk.Samia

Aidha Dk.Samia ametoa rai kwa wadau wote wanahusika na mapambano ya kuzuia na kupambana na Rushwa kutafakari na kuchambua kwa dhati masuala ya Rushwa ili kubainisha changamoto za mapambano hayo na kuchukua hatua muafaka huku akiwataka wala Rushwa kufahamu kuwa nchi za Afrika si chaka la kuficha fedha zilizotokana na Rushwa na kufuga wala Rushwa.         

Previous Post Next Post