AUAWA KWA KUSHAMBULIWA NA NYUKI NYUMBANI KWAKE

 

Na Fedrick Mbaruku 

MAMA mmoja mkazi wa Mtaa wa Mtakumbuka kata ya Momoka Edeni  Ng'ambo Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Janeth Swedi (72) ameuawa kwa kushambuliwa na nyuki akiwa nyumbani kwake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa mtaa huo Mohamed Makubi amesema tukio hilo la taharuki lilitokea majira ya jioni Julai 10,2023 ambapo amesema kuwa jitihada za kumuokoa bibi huyo zilifanyika akapelekwa hospitali lakini ilipo fika majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo julai 12 alipoteza maisha.

Aidha diwani wa kata ya momoka chalse chakupewa naye amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akiwataka Wananchi Mkoani humo kuondokana na imani za kishirikina.

Previous Post Next Post