NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA KWA MWAKA 2023

Na Fedrick Mbaruku 

Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2023.

Akitangaza matokeo hayo leo Julai 13 mwaka huu katika Ofisi hiyo  nchini Zanzibar Katibu wa NECTA Dkt.Saidi Mohamed amesema jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani ni 1,68,83 huku wasichana wakiwa ni 47,340 na wavulana ni 59,543 ambapo jumla ya watahiniwa ni 104,549 sawa na asilimia 99.23 ya watahiniwa waliofanya mtihani kwa mwaka 2023.

Katika hatua nyingine Mohamedi amesema mwaka 2022 waliofaulu walikuwa 93,136 sawa na asilimia 98.97 na kusema ufauli wa jumla kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 0.26 ikilinganishwa na mwaka Jana.

Previous Post Next Post