MAAGIZO YA DKT.MPANGO KWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA NA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU


MAAGIZO YA DKT.MPANGO KWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA NA a 
Fedrick Mbaruku

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Phlip Mpango amevitaka Vyombo vya Dolan a Mahakama kuendelea kusimamia utekelezaji wa haki na kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa mujibu wa hukumu na vifungu vya sharia.

Dk.Mpango ameyasema hayo hii leo Julai 22,2023 alipokuwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Ruvuma ambapo amezindua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi Mkoani humo.

Akiwa Mkoani Ruvuma Dk.Mpango amesema kampeni ya Legal Aid Campaign ijikite katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu haki za watu wenye ulemavu huku akisema kwa mjibu wa ibara ya 13 ya katiba ya 1977 inaeleza kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria.

“Wanayo haki bila ya ubaguzi wowote kulindwa nan a kupata haki sawa na mbele ya sharia,”Dk Mpango

Amesema kumekuwepo na ubaguzi na uonevu kwa watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali nchini na kusema watu wenye ulemavu wanatakiwa kupewa haki kama ilivyo kwa watu wasio kuwa na changamoto.

Sanjari na hayo Dk.Mpango ameonya vikali vitendo hivyo na kuitaka jamii kutambua kua walemavu wanahaki ya kuishi na kushiriki shughuli za jamii,kupata huduma za afya,elimu na kupata kazi na ajira.

Dk.Mpango amezielekeza Wizara ya Katiba na sharia kushirikiana na wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu kutoa elimu kwa jamii kusimamia utekelezaji wa sharia ya watu wenye ulemavu ya 9 ya mwaka 2010.

Pia amezipongeza wizara ya katiba na sheria kwa kushirikiana,taasisi za serikali,asasi za kirai kutoka pande zote za muungano.

Pia Makamu wa Rais amemuagiza waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Seleman Jafo kufanya uchambuzi wa kina wa masuala mbalimba ya kampeni ya Legal Aid Campaign (MSLAC) tangu kuanza kwake na kuyawekea mikakati wa kuyapatia ufumbuzi kubadili yatakayo  onekana kuwa kelo kwa wananchi ili kuleta haki na usawa kwa wananchi.

Pia amewataka wananchi wenye uhitaji wa musaada wa kisheria kutumia fursa hiyo kikamilifu huku akiwasihi wananchi wote kuendelea kutekeleza wajibu wao katika malezi ya watoto ulinzi wa haki za makundi maalumu,kutoa taarifa juu ya vitendo vya kiuhalifu na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya haki pindi unapohitajika na sikujichukulia sharia mkononi.

Aidha Dk.Mpango amewaagiza Viongozi wa Vijiji na Kata kuwa mstari wa mbele katika kutatua kero na changamoto kwa wananchi na kuonya suala la kusubili uongozi wa juu kupita.

“Naomba nitumie fursa hii kuwashukuru kwa dhati Viongozi na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kwa mapokezi mazuri mlionipatia.

Aidha Dk.Mpango ameupongeza Mkoa huo kwa jitihada zinazofanywa Mkoani humo katika shughuli za uzalishaji mali,kilimo,biashara,viwanda na huduma mbalimbali na kusema Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuwa tegemezi kwa Taifa katika uzalishaji wa chakula.    

Previous Post Next Post