MAAGIZO SABA YA WAZIRI MKUU MHE.KASIM MAJALIWA KWA VIONGOZI WA JESHI LA POLISI NCHINI

Na Fedrick Mbaruku 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa jeshi la polisi nchini,Wakuu wa vyombo vya usalama, kuhakikisha wanaandaa mpango mahususi wa mafunzo kwa askali wa kike ili kuwapatia mbinu za kukabiliana na changamoto za kijinsia katika utendaji kazi wao wa kila siku katika maeneo yao.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Julai,23,mwaka huu wakati wa ufunguzi wa kongamano la mafunzo ya shirikisho la kimataifa la polisi wanawake lililofanyika Jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu amewataka washiriki wa kongamano la mafunzo hayo kutumia fursa hiyo kusikiliza,kujifunza,kuzungumza,na kuchangia mada kwa yale wanayofundishwa ili kuwasaidia katika majukumu yao ya kila siku ili kuunga mkono shirikisho la kimataifa la polisi wanawake.

Amesema askali wa kike wanatakiwa kuwa chachu ya mabadiliko katika utendaji kazi wao na kuwa mfano kupitia mafunzo mbalimbali watakayoyapata kupitia kingamano hilo.

“Baada ya mafunzo haya mkatekeleze majukumu yenu kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu bila kusahau misingi ya utawala bora na maadili ya kazi yenu sambamba na kuboresha uhusiano wa wananchi na jeshi la polisi ili jamii iendelee kuwa na imani na jeshi letu la polisi na hii ni namna bora ya kufanikisha kwa vitendo kaulimbiu ya huduma za jamii kupitia uwezeshaji wa wanawake katika utekelezaji wa sharia.

“Suala la ulinzi liwe letu sote tukishirikiana na vyombo vya ulinzi nah ii ni kwaajili ya wananchi wote naomba nitumie nafasi hii kuwaasa watanzania na wadau mbalimbali kuthamini sana na kutambua kuwa utulivu wa nchi amani,umoja na mshikamano ni nguzo muhimu katika usitawi wa Taifa,”Waziri Mkuu Majaliwa

Aidha Waziri Mkuu amewasisitiza watanzania na wadau wote nchini kutambua na kuthamini utulivu wa nchi na kusema amani,umoja na mshikamano ni nguzo ya kiuchumi,kisiasa na kijamii huku akibainisha kuwa hali hiyo ni uhuru wa mawazo ya kila mtanzania alionao.

Amesema kufuatia kongamano hilo yapo manufaa mbalimbali ikiwemo kuimalisha usalama wa nchi,kuwajengea uwezo kwenye Nyanja mbalimbali za kutoa mafunzo yakiwemo ya jinsia,kuwaleta pamoja wanachama wa shirikisho la kimataifa la polisi wanawake,kuimalisha mtandao wa maofisa wa kike wa polisi kutoka pande mbalimbali za bara la Afrika,fursa ya kujifunza utamaduni mbalimbali ikiwemo masuala ya upendo amani na mshikaman pamoja na kuimalisha fursa ya kidiplomasia kati ya nchi wanachama wa kimataifa la polisi wanawake Barani Afrika na kupata maarifa yatakayoimalisha utendaji kazi ndani ya jeshi la polisi nchini.

Pia Waziri Mkuu ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kazi anayoifanya ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo nchini.

Sanjari na hayo pia amempongeza Kamishina wa jeshi la wanawake la polisi Suzan Kaganga kulitaka kutumia vema kaulimbiu ya kongamano hilo yam waka 2023 inayosema "Huduma kwa Jamii kupitia uwezeshaji wa wanawake katika utekelezaji wa sheria”kauli inayotajwa kuwajengea uwezo polisi wa kike ili kutoa huduma bora kwa wananchi.



Previous Post Next Post