Na Fedrick Mbaruku
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mioa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Angellah Kairuki ametangaza rasmi uchaguzi wa Wanafuzi kujiunga na kidato cha tano,Vyuo vya Ualimu,Vyuo vya Elimu ya Ufundi pamoja na Vyuo vya kati kwa mwaka 2023.
Waziri Kairuki ameyasema hayo Juni 11,2023 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI uliopo Jijini Dodoma.
Amesema zoezi hilo limefanyika kwa kuzingatia takwimu za matokeo ya wanafunzi ambao walifanya mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka 2022 ambapo limezingatia wanafunzi kutoka Tanzania Bara.
Waziri Kairuki amesema wanafunzi waliochaguliwa wanatoka katika shule za serikali,shule zisizo za kiserikali,watahiniwa wakujitegemea waliofanya mitihani chini ya taasisi ya elimu ya watu wazima pamoja na waliofanya mitihani chini ya vyuo vya maendeleo ya wananchi (FTCC).
Amesema matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2022 takribani ya watahiniwa 192,348 sawa na asilimia 36.95 walipata ufaulu wa daraja la kwanza mpaka daraja la tatu ambapo kati ya watahiniwa hao Tanzania bara kulikuwa na watahiniwa 188,128 ambapo kati yao wasichana ni 84,509 na wavulana ni 103,619 huku akisema wanafunzi wote wamekidhi vigezo vya kujiunga na kidato cha tano,Vyuo vya Ualimu,Vyuo vya elimu ya ufundi na Vyuo vya kati kwa mwaka 2023.
Pamoja na hayo Waziri Kairuki amesema idadi hiyo inawajumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu 490 ambapo kati yao wasichana ni 218 na wavulana ni 272 na kusema wanafunzi wote 188,128 wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali nchini pamoja na Vyuo vya fani mbalimbali.
Waziri Kairuki amebainisha mchanganuo wa wanafunzi hao ambapo amesema wanafunzi 129,830 wakiwemo wasichana 36,343 na wavurana 63,487 sawa na asilimia 69 wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kidato cha tano,Wanafunzi 1878 wakiwemo wasichana 1097 na wavulana 781 wamepangiwa katika shule maalumu 8 ikiwemo shule ya Kilakara,Mzumbe,Igoru,Kismiri,Msalato,Kibaha,Tabora Boys na Tabora Girls.
Amesema Wanafunzi 122,908 wakiwemo wasichana 62,731 na wavulana 60,177 wamepangiwa katika sekondari za bweni za kitaifa za kidato cha tano wakati wanafunzi 5,044 wakiwemo wasichana 2,515 na wavulana 2,529 wamepangwa katika shule za sekondari za kutwa za kidato cha tano.
Katika hatua nyingine Waziri Kairuki amesema kuwa Wanafunzi 58,298 ambapo kati yao wasichana ni 14,166 na wavulana ni 40,132 ambao ni siwa na asilimia 31 wamepangiwaa kujiunga na kwenye kozi mbalimbali za stashada katika Vyuo vya kati vinavyosimamiwa na baraza la elimu ya ufundi (NACTEVET).
Wanafunzi 1,645 wakiwemo wasichana 646 na wavulana 999 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Ualimu ngazi ya Stashahada ya sayansi Hesabu pamoja na Tehama huku akisema wanafunzi wa Vyuo vya kati Wanafunzi 1,877 wakiwemo wasichana 757 na wavulana 1,120 wachaguliwa kujiunga katika fani mbalimbali katika Vyuo 4 vya elimu ya ufundi kiwemo Chuo cha Ufundi cha Arusha,Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (BIT),Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUC),Chuo cha Usimamizi na Maendeleo ya Jamii Maji (WDMI).
Pia ameeleza kuwa Wanafunzi 1,842 wakiwemo wasichana 943na wavulana 899 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya afya kwa ngazi ya stashahada wakati wanafunzi 52,934 ambapo kati yao 15,820 na wavulana 37,114 wamechaguliwa kujiunga katika kozi mbalimbali zikiwemo kozi za kilimo,Ufugaji,Utawala,Biashara za stashahada katika Vyuo vya kati mbalimbali nchini.
Waziri Kairuki amesema katika muhula wa kwanza kwa kidato cha tano unatarajia kuanza Agosti 14,2023 huku akiwataka Wanafunzi wote waliopangwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka huu wanatakiwa kuwasili katika shule walizopangiwa kuanzia Agosti 13,mwaka huu na siku ya mwisho ya kuwasili ni Agost 31,2023.
Sanjari na hayo Waziri Kairuki amebainisha idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano ni 129,830,wanaojiunga na makundi ya Vyuo vilivyoainishwa ni 58,298 ambapo jumla ni 188,128 kwa walio pata daraja la kwanza hadi daraja la tatu.
Katika hotuba yake Waziri Kairuki amewapongeza wazazi,walezi na walimu kote nchini kwa juhudi mbalimbali walizozifanya hasa katika ufundishaji wa na namna walivyowawezesha wafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.
Aidha Waziri Kairuki ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanaitekeza adhima ya Serikali ya kuwa na shule za sekondari za kidato cha tano katika kila tarafa ili kuwawezesha wanafunzi wanaofaulu mtihani wa kidato cha nne waweze kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano na kidato cha sita.
“Nitoe rai kwa wazazi na walezi tuendelee kuwa na moyo wa kuwasimamia na kufuatilia maendeleo ya watoto wetu na niwapongeze sana wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano,Vyuo vya Ualimu na vya kati nitumie pia fursa hii kujituma katika kujifunza zaidi ili waweze kufanikiwa kujiunga na mafunzo ya elimu ya juu pindi watakapohitimu kidato cha sita.
“Upanuzi na ujenzi wa shule mpye za kidato ch tano na cha sita ni vema ukaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza taasusi zaidi za masomo ya sayansi vile vile mikoa ni vema ikahakikisha inakuwa na taasusi zote za msingi katika shule zake ili kuwapunguzia wazazi wetu na walezi ghalama za usafiri kuelekea wanafunzi kwenda katika shule za mbali,”Waziri Kairuki.