Na Sophia Paul
Timu ya soka ya ya Chihondo fc imendeleza ubabe kwenye uwanja wa nyumbani kwa kutembeza kichapo cha mabao 2-1 Akata fc katika mchezo wakirafiki uliochezwa katika dimba la chihondo lililopo kata ya nala Jijini Dodoma.
Akizungumza na Maulus Media Kocha wa timu ya Chihondo fc Maneno Hassan alisema walijiandaa vizuri kukabiliana na mchezo huo pamoja na mbinu alizo wapa wachezaji kwenye uwanja wa mazoezi ndizo zilizoweza kuwapa ushindi.
Alisema mchezo huo ulikuwa maalumu kwao kwa ajili ya kupima uwezo wa wachezaji wa timu hiyo ambayo inatarajia kushiriki kwenye ligi ya Mbuzi Cup inayo tarajia kuanza juni 20,2023 kwenye uwanja wa Chihondo .
“Niliwambia wachezaji wangu wacheze kwa utulivu na nidhamu ili wapinzani wetu wasiweze kupata na motokeo kwenye uwanja wetu wanyumbani na nashukuru kile kitu nilicho wa eleza ndicho walicho kifanya na kimezaa matunda.
“Pia niliwaambia vijana wajitume na waondoe hofu kwenye mchezo wasiogope kwa kuwa timu hiyo inanatokea Dodoma Mjini ndiyo tutoke kwenye mchezo bali wachezaji wamejituma kwa sababu panapo jitihada kuna mafanikio”Alisema Hassan
Kwa upande wake kocha wa Timu ya Akata fc ajulikanaye kwa jina la Don Mandonga alisema walishindwa kupata matokeo kwenye mchezo kutokana na wachezaji wa timu yao kuwa na hofu ya mchezo kitu ambacho kimewafanya kuondoka wakiwa wameinamisha vichwa chini.
Alisema timu yao ilisafiri umbali mrefu na wachezaji walifika wamechoka kitu ambacho kilipelekea timu hiyo kuingia uwanjani bila kufanya mazoezi ili kuuzoea uwanja huo.
Mandonga alisema mabao mawili ya kipindi cha kwanza yaliyo fungwa na Richard Michael dakika ya 23,44 ya liweza kuwatoa mchezoni na kuwa sababisha wakate tama.
“Nawaomba wachezaji wangu wasikate tama kwa kuwa tumeshindwa kupata matokeo ugenini tutarudi kwenye viwanja vya mazoezi ili kulekebisha makosa ambayo tumyafanya ili yasiweze kujirudia kwenye michezo inayofuata”alisema Mandonga