NAIBU Waziri wa kilimo na (Mb) wa Dodoma Mjini
Mhe.Antony Mavunde amewataka akinamama wajasiliamali kuchangamkia fursa
mbalimbali za kiuchumi ili kuleta mabadiliko chanya katika taifa na jamii kwa
ujumla.
Mhe.Mavunde ameyasema hayo hii leo Juni 9,mwaka huu
wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye semina ya akinamama wajasiliamali katika
hafla ya uzinduzi wa program ya “She can do it” iliyohusisha ugawaji wa hati za umiliki wa ardhi iliyofanyika
katika ukumbi mdogo uliopo PSSSF Jijini Dodoma.
Amesema kwa mjibu wa sheria ya manunuzi ya umma
iliyofanyiwa marekebisho anaelea bayana kuwa taasisi zote nunuzi zinatakiwa
kutenga asilimia 30 ya manunuzi yake ya ndani kwa lengo la kuyainua makundi
maalumu wakiwemo akinamama,vijana na watu wenye ulemavu.
Amesema katika ujenzi wa mji wa serikali Jijini humo zimeingia
shilingi Bilioni 300 ambazo zipo kwenye mzunguko zitakazo tumika katika ujenzi
wa mji wa serikali zinazotoa fursa mbalimbali kwa akinamama wajasiliamali,vijana
na watu wenye ulemavu.
“Fursa hizi zipo lakini je wakowapi hao watu
wakufanya hivo nataka niwaombe mama zangu ya kwamba tuzichangamkie hizi fursa
na inawezekana kabisa tunayo miradi mingi hapa Dodoma na kama mko teyari mimi
Ofisi ya Mbunge iko wazi na niko teyari kumshika mtu mkono nikampeleka sehemu
husika akaendelea na mpango huu uliopo.
Mhe.Mavunde amesema Dodoma ndio sehemu pekee kusini
mwa jangwa la sahala huku akibainisha kuwa kunaujenzi wa barabara ya mzunguko
yenye kilometa 112.3 ambayo itakuwa na takribani njia nne itakayo chochea
maendeleo katika Jiji la Dodoma na maeneo mengine hapa nchini.
Hata hivyo Mhe.Mavunde amepanga kuwalipia akinamama wajasiliamali
ghalama za kujiunga katika suala zima la ujasiliamali ili kushiriki katika
maonesho ya sabasaba yanayotarajia kufanyika July 7,mwaka huu huku akisema
akinamama wanao wigo mpana wa kubadilika kiuchumi.
Amesema kutokana na ujenzi wa uwanja wa Ndege wa
kimataifa uliopo Jijini humo unatarajia kuleta fursa itakayowawezesha
wajasiliamalia kusafiri biashara zao kwa urahisi hali ambayo itawafanya kuendesha shughuli
zao kwa ufanisi.
Mhe.Mavunde amesema Reli itakapo kamilika kutakuwa
na uwezekano wa kusafirisha biashara zao kwa haraka sana na kwa muda mchache huku
akiahidi kuwaunga mkono akina mama wajasiliamali Jijini humo.
“Kwa haya anayoyafanya Mama yetu Dk.Samia Suluhu
Hassan labda mshindwe nyie na mimi niko teyari kumsaidia mtu yeyote atakae
hitaji msaada kwa ajiri ya kukuza na kuleta maendeleo.
“Nimetoa ofa kwa mfanyabiashara yeyote kupitia sido
nitatoa shilingi Milioni 20 kila mwaka ili nitakapoondoka kiwepo kitu
kitakachoonekana na kikumbukwe kuwa na Fulani aliacha hiki,”Mhe Mavunde
“Hakuna mtu anaepewa rifti akiwa amekaa nyumbani
kwake jamani ukitaka rifti sogea barabarani ebu sasa hivi tuanze kumnyenyua mtu
mmoja mmoja tuone ili kesho na keshokutwa tuone mafanikio yao.
Nae Festa Mbaga kutoka kampuni ya Akili mia ametoa
wito kwa akina Mkoani humo kujua mahali,hatua mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa
ili kupata mikopo na namna ya kurejesha katika taasisi mbalimbali za kifedha
hususani katika Benk.
Mbaga amewasihi akinamama hao kuwa waaminifu katika
sehemu wanazokopa fedha hizo huku akionya tabia ya watu kukopa kasha kasha kutokomea
kusiko julikana ba badala yake kujenga uaminifu ili kufikia hatua kubwa zaidi
katika kutimiza adhima aliyojiwekea mhusika.
Amoni Mabusi ambae ni Meneja wa Benki ya NMB tawi la
Dodoma na Kanda ya kati amesema wajasiliamali wengi si watanzania pekee ambapo
wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mitaji huku akiwasihi wajasiliamali
kuwa na lughu nzuri ya kibiashara hali ambayo inaweza kukufanya biashara
isikuwe.
Amesema katika suala la ujasiliamali biashara
inahitaji usimamizi wa hali ya juu na kusema mara nyingi wasimamizi na
wataalamu wa biashara wanashauri kuwa unatakiwa kuwa msimamizi wa karibu katika
biashara.
Pia amewashauri kuwa makini katika majanga ya
kibishara yanayoweza kujitokeza pindi mfanyabiashara anapoendesha shughuli zake
ikiwa ni pamoja na majanga ya moto,wizi,kunyeshewa na mvua kasha kutafuta
suluhisho kwa haraka juu ya majanga hayo.
“kama unaduka ni la milioni 20 halafu likaungua
maana yake milioni 20 zimeungua sasa maana yake ni kwamba unatafuta milioni 20
tena usimamishe biashara kama ile kwahiyo kuna haja kubwa ya kuitengenezea lisk
ili ikitokea usije ukatafuta hela nyingineza kufidia pale unaweza ukawa na bima
na mengine.