SERIKALI Kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepanga kutekeleza Ajenda ya maendeleo endelevu ambayo pamoja na Mambo mengine imeainisha malengo 17 ya Maendeleo ambayo kwa kifupi yanajulikana Kama SDGs malengo hayo yanaonesha shabaha ambazo Dunia inategemea kufikia ifikapo mwaka 2030
Tanzania inapaswa kuwasilisha katika jukwaa kuu la kisiasa nchini marekani V.N.R mchakato wa kufanya utafiti wa SDGs linajumuisha sekta zote pamoja na taasisi "ameeleza Jennifer
Naye Naibu Katibu Mkuu wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw Frank Rozamula amesama kutokana na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu wizara ya Elimu inagusa kila mtu na inazingatia ubora wa Elimu na inwafikia na kuwafikaa watanzania
"Wizara ya elimu tumefanya Mambo mengi Kwanza tumejenga miundombinu Kama madarasa kwa shule za msingi na shule za sekondari ilikuhakikisha watoto hawapati shida sehemu ya kujifunzia pamoja na vitabu lakini tumetoa mafunzo kwa walimu walio shuleni na walio mafunzoni tumetoa vishikwambi kwa walimu,
"kwa upande wa elimu ya juu tumejenga kampasi 17 katika mikoa minne ilikufikia maeneo ambayo hayana vyuo vya Kati na kila mkoa tumepanga kujenga shule ya watoto wa kike na kila shule itakuwa wa wanafunzi 1000"ameeleza Rozamula