MHE.NAPE:HATAKAMA MBEGU NI NDOGO NAMNA GANI IKIPUUZWA IPO SIKU ITAOTA NA ITAATHILI TAIFA LETU

 

Na Fedrick Mbaruku

WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye amewataka watanznia kuacha upotoshaji unaoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na kuondoa hofu juu ya suala la makubaliano ya mkataba baina ya Tanzania na DP World (Dubai).

Waziri Nape ameyasema hay leo Juni 10,2023 Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akichangia hoja kuhusiana na sintofahamu iliyotanza katika vichwa vya watanzania wengi kuhusu makubaliano ya mkataba wa Bandari ya Dar es salaam na kusema wanatakiwa kuondoa hofu juu ya suala hilo.

“Mhe.Sipika ukiacha watu wachache kwa mtu aliyetaka kuelewa kuhusu hili hofu imeondoka kama kuna mtu walikuwa na mashaka na uzale,uthabiti na uimara wa Bunge hili bilashaka leo tumethibisha hili ni Bunge imara sana maana upepo ulivyokuwa unapulizwa walidhani watu watayumba hapa.

“Wapo watu wachache ambao walitaka kutumia hofu hii kujalibu kulikoroga Taifa letu na hawa vizuri tuakashughulika nao kwa sababu mbegu hata kama ni ndogo namna gani ikipuuzwa ipo siku itaota itaathili Taifa letu na kwenye hili ni vizuri tusiyumbishe maneno tusimumunye maneno hawa tuwakabili usoni mchana peupe,”Waziri Nape

Mhe.Nape amesema malidhiano ya mkataba huo yasitumike kuligawa Taifa huku akiwataka viongozi wa serikali kulaani vikali suala hilo kwa kuzingatia ulinzi na maslahi mapana ya Taifa.

Hata hivyo kufuatia mjada wa mkataba huo uliojadiliwa Bungeni hii leo Jijini Dodoma,Bunge limepirisha rasmi makubaliano ya mkataba huo.

Previous Post Next Post