Na Fedrick Mbaruku
SERIKALI imetia saini mikataba ya kupeleka huduma za mawasiliano nchini baina ya mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) na watoa huduma za mawasiliano nchini.
Hayo yamesemwa juni 28 mwaka huu Bungeni Jijini Dodoma na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa ambapo alisema mikataba hiyo itawezesha kujengawa kwa minala 758 katika kata 713 hali ambayo itasaidia kuimarisha mawasiliano katika maeneo hayo.
Waziri Mkuu alisema mikataba hiyo inathamani ya shilingi bilioni 265.3 huku akisema hadi sasa serikali imekamilisha malipo ya fidia kwa wananchi 1,142 waliotoa maeneo yao ili kupisha utekelezaji wa mradi huo hasa katika maeneo ya Ligangana na Mchuchuma Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe ambapo kiasi cha fedha shilingi bilioni 15.4 zimetolewa.
Alisema malipo hayo yamejumuisha fidia pamoja na riba ya miaka saba tangu wananchi hao 16 walipofanyiwa tathimini juu ya mradi huo.
“Nimpongeze Rais kwa hatua hiyo muhimu,niwaombe wananchi waendelee kuiunga mkono serikali katika utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu,”Waziri Mkuu
Pia Waziri Mkuu alisema serikali imeendelea kuimalisha kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua Ndege kubwa ya kubebea mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 54 kwa wakati mmoja ambayo itasaidia kuongeza kasi na uwezo wa usafirishaji wa bidhaa mbalimbali na mazao kwenda nje ya nchi.
“Nilihakikishie Bunge lako tukufu kuwa serikali impokea maoni na michango yote na baada ya kuthibitishwa kwa mkuutano huu itasimamia ipasavyo utekelezaji wa bajeti hii,”Waziri Mkuu