MBARAZA WA WILAYA YA MPWAPWA JIJINI DODOMA AHUDHULIA MKUTANO WA HADHARA

 


Na Ramadhani Mtapila

MBARAZA wa Wilaya ya Mpwapwa iliyoko Jijini Dodoma Aminael Meshack Sayango amehudhuria mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Nudgu Daniel Chongolo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Dodoma.

Mkutano huo umefanyika Juni 25,2023 katika uwanja wa Mtekelezo Jijini Dodoma ambapo umehusisha viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu mstaafu Mhe.John Malechela,Naibu waziri wa kilimo ambae pia ni Mbunge wa Wilaya ya Dodoma mjini Mhe.Antony Mavunde,Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso,Waziri wa ardhi Dkt.Angeline Mabula,Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe.Deo Ndejembi,Mwenyekiti wa umoja wa vijana Taifa Ndugu Mohamed Ali Kawaida na viongozi wengine wa Chama hicho.

Katika ziara yake Katibu Mkuu Ndug.Chongolo amekagua na kuzindua miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa kiwanda cha mbolea,Barabara ya mzunguko,Mradi wa maji pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi Mkoani humo

Previous Post Next Post