RAIS SAMIA AWATAKA WATANZANIA KUWA WAZALENDO KATIKA MICHEZO

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania na mashabiki wa michezo kuweka mbele uzalendo katika michezo kwa maslahi ya Taifa.

Dk.Samia ameyasema hay oleo Juni 5,2023 wakati wa hafra ya chakula cha usiku ya kuipongeza Timu ya Yanga kwa hatua waliyoifikia ya kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF)iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete,Ikulu Jijini Dar es salaam.

Rais Samia amesema Timu yoyote itakayoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya michezo ya kimataifa ichukuliwe kama Timu ya Taifa na utani wa jadi ufanyike katika mechi za nyumbani pekee.

Hata hivyo amesema hatua ya Timu ya Yanga kufika kwenye mashindano ya CAF imeleta heshima na kurejesha nchi katika ramani ya kisoka na michezo kwa ujumla.

Rais Samia amesema Serikali itaendelea kufanya jitihada katika michezo ili kuiwezesha nchi kukaa kwenye ramani ya michezo Duniani.

Pia amewapongza wapenzi na mashabiki wa timu ya Yanga kwa hamasa waliyokuwa wakiitoa kwa wachezaji wa Yanga wakati wa mashindano hayo.

Aidha Dk.Samia ametoa wito kwa Serikali za mitaa kote nchini kuweka mkazo katika michezo na kuwa na viwanja katika maeneo yao.

 

 

Previous Post Next Post