Wazir Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa Ofisi 2018 na kufungua mafunzo
kwa Mawakili wa Serikali yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya
Kikwete Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amezielekeza Wizara,Idara na Taasisi
zote kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika
uendelezaji wa mashauri hayo huku akizitaka Taasisi za umma zenye Mawakili wa
Serikali kuzingatia utatuzi wa kero za Wananchi ili kupunguza mlundikano wa
mashauri ambayo hayana ulazima wa kufikishwa Mahakamani.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe
Jaji .Dkt.Elieser Feleshi amesema uamzi wa kuanzisha Ofisi hiyo ni kuimalisha
sekta ya sheria nchini hususani katika kuongeza ufanisi zaidin katika uendeshaji
wa mashauri ya madai na usuluhishi nchini.
Amesema hatua hiyo imeisaidia Serikali kuokoa fedha
nyingi ambazo zinaenda kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo nchini kwa
manufaa ya Taifa.
Katika hatua nyingine ameeleza kuwa kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Ofisi yake na Ofisi
ya Wakili Mkuu wa Serikali,Mhe.Jaji
Yohane Massara,Jaji kiongozi Mahakama ya Afrika Mashariki amasema Ofisi yake
itaendelea kutoa ushirikiano ili kufikia hatua kubwa zaidi.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyemule
ameipongeza Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa utendaji kazi mzuri na
kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa
dhamira aliyonayo kwa kila sekta ikiwa ni pamoja na sekta ya sheria na taasisi
zake katika kuahakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na haki kupitia vyombo vya
kisheria hapa nchini.