Prof.Makame Mbarawa ameyasema hayo hii leo Mei
3,2023 katika hafla ya mapokezi ya Ndege ya mizigo aina ya Boelng 767-300F
iliyongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal One) Jijini Dar
es salaam.
Amesema Serikali kupitia Wizara hiyo imekuwa ikitoa
kipaumbele katika kughalamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
nchini.
Prof.Mbarawa alisema ujio wa Ndege hiyo utaenda kuwa
chachu ya biashara kati ya Tanzania na mataifa mengine na kusema adhima hiyo
itaendana na utekelezaji wa farsafa ya Dipromasia ya uchumi ambayo imekuwa
ikisisitizwa na Mhe.Rais Dk.Samia Suluhu Hassan sambamba na mahusiano kati ya
Tanzania na mataifa mengine Duniani.
Alisema Wizara itaendelea kutekeleza majukumu yake
makuu na kuandaa sera zitakazo saidia matumizi ya rasilimali kupitia uwekezaji
unaofanywa na serikali ili kuleta matokeo chanya katika ukuaji wa shughuli za
kiuchumi nchini.
Sanjali na majukumu hayo Prof.Mbarawa alisema Wizara
itaendelea kujenga mazingira wezeshi katika sekta za kiuchumi na kijamii na
sekta binafi katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weredi wa hali ya
juu.
“Sekta ya usafilishaji inaleta uhai katika shughuli
za kiuchumi kama ilivyo damu katika mwili wa Binadamu.
“Kwa kutambua hilo tutaendelea kushirikiana na sekta
binafsi zinazo zalisha mizigo ili kuhakikisha mizigo hiyo inafika kwa haraka
katika masoko mbalimbali Duniani,”alisema
Alisema Wizara hiyo kupitia Serikali itaendelea
kusimamia uboreshaji wa Viwanja na miundombinu mbalimbali ili kuwezesha
mashirika ya Ndege ndani na nje ya nchi kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi
zaidi.
Aidha Prof.Mbarawa aliishukuru na kuipongeza
Serikali kwa kuendelea kuiboresha ATCL katika nyanja mbalimbali za kusafirisha
abiria na mizigo.
Akitoa taarifa ya Ndege hiyo Mtendaji Mkuu wa ATCL
Lardslaus Matindi alisema mpango wa Ndege za mizigo umelenga kurahisisha
usafirishaji wa bidhaa kutoka na kuingia nchini.
Alisema katika kutekeleza mpango mkakati wa pili wa Kampuni ya Ndege Tanzania
ndani ya kipindi cha miaka mitano kwa mwaka wa fedha 2022/2023 hadi 2026/2027
inatakiwa kuwa na Ndege takribani 20 zikiwemo ndege za masafa mafupi 8,masafa
ya kati 8,masafa marefu 3 na Ndege moja kubwa ya mizigo.
Aidha Matindi Alisema mapokezi ya Ndege hiyo
kumeifanya ATCL kuwa na Ndege 13 zilizopo nchini na Ndege tatu zikiendelea
kuundwa wakati Ndege mbili kati ya hizo tatu aina ya Boelng 737-9MAX zinztzrzjiwa kuwasili
nchini kati ya mwezi wa nane na mwezi wa 12 mwaka huu huku Ndege ya tatu Boelng
787-8 ikitarajiwa kuwasili 2024.