Itakumbukwa Mei 5 mwaka huu DOMECO ilichuana na timu ya Homeboys katika uwanja wa Shule ya Msingi Kazikazi na leo Timu hizo zimekutana kwa ajiri ya mchezo wa kirafiki Jijini Dodoma..
Mchezo huu umechezwa
leo Mei 2 2023,katika uwanja wa Shule ya Sekondari City uliopo Jijini Dodoma
ambapo katika mchezo huo timu zote zikiwa na ushindi wa bao 1-1 Homeboys wakitangulia
kupata gori la kwanza katika kipindi cha kwanza dakika ya 42 lililofungwa na
mchezaji Yohana Jackson huku DOMECO wakifuatia kupata gori katika kipindi cha
pili lililofungwa na Barakia Bosco Iputa.
Michuano hiyo inakuja
mala baada ya DOMECO kuifuata timu ya Homeboys ya Itigi Mkoani humo mchezo
uliochezwa Mei 5 mwaka huu ambpo DOMECO walitoka na ushindi wa bao 2-1,na leo
Itigi imefunga safari kuifuata DOMECO Jijini Dodoma na na kutoka sale ya bao
moja kwa moja na hadi kutamatika kwa mchezo huo timu zote zikiwa na majeruhi
mmoja.
Akisimulia mtanange huo
Nahodha wa timu ya DOMECO Barakia Iputa amesema kilichosaidia wao kurudisha
gori ni matumizi ya mbinu walizokuwa nazo huku akisema mpira ni mbinu.
“Kutangulia kufungwa
sio sababu kitu unachotakiwa ufanye ni mentainence walishazowea kutufunga gori
la kwanza tunachomoa tunawapiga kwahiyo mchezo kama huu wa leo wametufunga gori
la kwanza lakini tumewasoma akili yao maneno mengi vitendo hakuna.