Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philp Mpango ameliagiza Baraza la Taifa la Uhifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na mamlaka za Serikali za mitaa nchini kote kusimamia na kuongeza nguvu katika utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki.
Dk.Mpango ameyasema hayo mapema hii leo Juni 05,2023
alipokuwa akizungumza na wananchi katika viunga vya Soko la Machinga Complex
Jijini Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira Duniani.
Amesema Mamlaka zinatakiwa kuchukua hatua za
kisheria kwa wale wanaoenda kinyume na maagizo ya ya Serikali katika kusimamia
vyema suala la matumizi ya mifuko ambayo haija thibitishwa huku akiwataka
watendaji wanao husika kusimamia kwa ukaribu uzalishaji wa mifuko mbadala.
“Tuache mazoea ya kutupa taka ovyo sio usitaarabu
kufanya kila eneo liwe jalala la kutupa taka ni lazima sasa tujenge mazoea ya
kuyaweka mazingira safi na kwa wale walioko mazingira ya mjini ni vema kila
kaya iwe na sehemu mahususi ya kuhifadhia taka au kuchoma taka,”Dk,Mpango amesema
Pia Dk.Mpango amezitaka Kampuni na watu binafsi
wanaozalisha bidhaa za plastiki kuahikisha wanakusanya taka zinazozalishwa na
kuondolewa huku akisisitiza suala la utupaji taka kiholela.
Katika hatua nyingine Dk.Mpango amesema kwa mjibu wa
kifungu cha 89 sheria za Serikali za
Mitaa,mamlaka za miji sura ya 288 Halmashauri zimepewa mamlaka ya kutunga sheria
ndogo za utunzaji wa mazingira na udhibiti wa taka.