SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo imesema itaendelea kutoa ushirikiano katika matamasha ya michezo na sanaa kwa ujumla yanayofanywa na watu mbalimbali nchini ili kuendelea kujenga jamii bora na yenye kuleta manufaa na tija kwa Taifa katika sekta ya Utamaduni,sanaa na michezo nchini.
Hayo yamesemwa Juni 23,2023 na Mkurugenzi msaidizi anayehusika na masuala ya haki na maendeleo ya Wasanii nchini Dkt.Asha Sali Mshana ambaye alikuwa mgeni rasmi alipomuwakilisha Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma katika tamasha la kumtafuta mtanashati na mlimbwende wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Dodoma lililofanyika katika Ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma.
Katika hotuba yake Dkt.Mshana alisema mashindano hayo ni miongoni mwa juhudi za kuunga mkono adhima ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan huku akisema mashindano hayo yataiwezesha Wizra ya utamaduni sanaa na michezo kutangaza utamaduni wa jamii ya kitanzania ukiwemo utamaduni wa mavazi kutoka katika makabila mbalimbali nchini.
“Naomba mtambue kitu wanacho kifanya sio uhuni tumeona vijana wengi wakipata ajira kupitia makampuni mbalimbali,kutangaza makampuni kupitia mashindano haya ya utanashati na ulimbwende.
“Tuwape ushirikiano vijana wetu katika kukuza vipaji vyao sanaa ni pan asana,sanaa hii ya ubunifu wa mavazi ni aina ya sanaa ambayo inakuwa kwa kasi sana na kuleta manufaa mengi kwa vijana wetu wa leo,”Dkt,Mshana alisema
Dkt.Mshana alisema Wizara imekuwa ikishiriki kikamilifu kwenye mashindano mbalimbali ya sanaa na michezo kwa ujumla ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na kusema Wizara inaahidi kuipa nguvu tasinia ya utanashati na ulimbwende.
Alisema lengo la mashindano hayo ni kufungua mianya ya upatikanaji wa fursa za ajira kwa vijana hususani walioko vyuoni hali ambayo itarahisisha vijana wengi kuingia mikataba mbalimbali.
Katika hotuba yake Dkt.Mshana alisema katika mashindano yaliyofanyika mwaka 2022 DOMECO walishiriki na kujipatia zawadi ya mshindi wa tatu pamoja na taji la Miss Poplality katia shindano la Miss Kahama wakati mwaka 2022 DOMECO walishiriki na kupata ushindi wa taji la Miss na Mr kwenye shindano la “THE NEXT SUPER STAR” lililofanyika Mkoani Morogoro.
Sanjari na hayo Dkt.Mshana alibainisha changamoto zinazowakabili waandaaji wa mashindano hayo ikiwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti,ukosefu wa fursa za kushiriki mashindano makubwa pamoja na mwamko mdogo wa wazazi na walezi juu ya kuibua vipaji vya vijana wao huku akiwaasa wazazi kuwa na mwamko katika kutambua na kuibua vipaji vya watoto wao.
“Nitumie fursa hii kuupongeza uongozi wa Chuo kwa kuendeleza mpango mkakati wenu wa kuhakikisha tasinia hii ya utanashati na ulimbende ndani ya Chuo hiki unakuwa endelevu.
Pia alisema Serikali kupitia Wizara hiyo inatoa rai kwa wazazi na walezi,jamii,vyuoni na watanzania kote nchini kuunga mkono vipaji vya vijana ili kuendelea kujenga jamii yenye kuleta tija kwa Taifa.
Nae Mkuu wa Chuo hicho Idrisa Abbakar alisema tangu kuanzishwa kwa Chuo mwaka 2017 yamefanyika matamasha matano ambapo kimekuwa kifanya vizuri katika taaluma na michezo kwa ujumla huku akisema Chuo hicho kimetoa zao la Waandishi wa Habari walioko kwenye vyombo vya habari tofauti hapa nchini.
Alisema kupitia mashindano yaliyofanyika yapo manufaa yaliyo patikaana kupitia matamasha ya utanashati na ulimbwende ni viashiria vinavyoweza kuwapa uwezo wa kujipatia kipato.
Mkuu huyo alisema pamoja kufanikisha shughuli hiyo bado kunachangmoto katika eneo la mavazi ikiwa ni kukosekana kwa wadhamini wanaotakiwa kuweka nguvu katika eneo hilo,fikila potofu za wazazi na walezi wao wakidhani ni uhuni hali inayofanya wengine kutokushiriki kutokana na mambo wanayokatazwa wakiwa majumbani kwao.
Adha Abbakar aliiomba Serikali kuweka nguvu katika sekta hiyo ili kuibua vijana wengi wanaoweza kupata fursa za ajira na kupunguza vijana wanaolalamika kuhusu ajira kila iitwayo leo huku akitoa wito kwa Dkt.Mshana na Wizara kwa ujumla kuendelea kutoa elimu kwa wazazi.
Kwa upande wa washiriki wa Shindano hilo waliopata ushindi wa Mtanashati na Mlimbwende walisema wamejisikia vuzuri baada ya kupata mataji ya ushindi kufuatia matumizi mazuri ya mbinu walizokuwa wakifundishwa pindi wakiwa katika mazoezi yao.
Waliotangwazwa rasmi kuwa Miss na Mr.DOMECO ni Valerria Adam na Fanuel Stephine wengine ni Zubeda Said Miss mshindi wa pili,Alfa Mwilawi Mr.namba mbili,Edita Chiwaligo ambae ni Miss mshindi wa tatu na kipaji(Talent),Sebastiani Ejide Mr.mshindi wa tatu na kipaji(Talent),Daud Malejee Mr.mwenye muonekano mzuri(Poplality) Jackson Juma Muonekano mzuri kwenye picha (photogenic),Dolice John muonekano mzuri kwenye picha (Photogenic),Janeth Gerard Miss top modal na Emmanuel Mosha Mr. top Modal.