Na Ramadhan Mtapila
KATIBU wa Chama cha Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Dodoma Mjini Ndugu.Isack Ngongi amewataka wananchi wote Mkoani Dodoma na watanzania wote kushiriki katika mkutano mkuu wa hadhara utakaoongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndg.Daniel Chongolo.
Ngongi ametoa wito huo hii leo Juni 23,2023 katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma Mjini alipokuwa akizunguza na Maulus Media ambapo amesema Mkutano huo unatarajia kufanyika Juni 25,2023 kuanzia majira ya saa 2:00 asubuhi katika uwanja wa Shule ya Msingi Mtekelezo uliopo Jijini Dodoma.
Akieleza juu ya maandalizi ya mkutano huo Ngongi amesema Katibu Mkuu anatarajia kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Kiwanda cha mbolea,mradi wa maji uliopo kata ya Nzuguni,Barabara ya mzunguko iliyopo Nala itakayo saidia kuondoa msongamano wa magari katikati ya Mji.
“Jambo litakuwa kubwa sana na makundi mbalimbali yatahudhulia hapa kwa hiyo niseme tu kwamba sisi jumuiya ya Umoja wa Vijana chini ya Mweneyekiti wetu Shaban Shaban tumejipanga vizuri na maandalizi yamefikia asilimia 100 ndio maana ukiangalia nje bendera zimetapakaa mji mzima.
Pia Katibu amewataka Vijana kutoka kata,wilaya zote Mkoani humo kujitokeza katika maandamano ya kuhamasisha Mkutano huo huku akiwatakaribisha wafanyabiashara wakiwemo wamachinga,Wanafunzi wa Vyuo pamoja na Waendasha Pikipiki(Bodabo