BUNGE LAPITISHA HOJA YA MAKUBALIANO YA MKATABA KATI YA TANZANIA NA DP WORLD (DUBAI)

Na Fedrick Mbaruku

WAZIRI wa ujenzi na uchukuzi Prof.Makame Mbarawa amewasilisha pendekezo la makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu ushirikiano na uboreshaji wa utendaji kazi katika bandari ya Tanzania iliyopo Jijini Dar es salaam ili kuongeza ufanisi wa bandari na kuwa shindani. 

Prof.Mbarawa ameyasema hayo leo Juni 10,2023 Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha hoja ya makubaliano ya mkataba wa bandari ya Dae es salaam baina ya Tanzania na Dubai ambapo  amewahakikishia watanzania kuwa Serikali imejipanga kuweka muda wa marejeo kwa kila mradi pamoja na kuweka viashiria muhimu vya ufanisi wa kiutendaji

Amesema Tanzania imewekeza kiasi cha fedha shilini trilioni 1 katika bandari ya Dar es salaam huku akibainisha kuwa bandari zinakabiliwa na changamoto ya ufanisi.

“Kitengo chetu cha makasha zile gati namba 5 mpaka namba 7 ambayo inahudumia ambapo mwaka jana ilihudumia takribani makasha laki moja na hamsini.

Waziri Mbarawa amesema bandari ya Dar es salaam ndio lango kuu la uchumi wa Taifa kwani asilimia 37 sawa na Trilioni 7.78ya makusanyo ya mapato ya TAR yanakusanywa kupitia bandari zilizopo nchini hasa katika bandari ya Dar es salaam.

AProf.Mbarawa amesema zipo sababu zilizofanya utendaji wa bandari hiyo kuwa dhaifu ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwekeza kwenye mitambo mikubwa ya kushushia makontena kwenye meli,changamoto ya mifumo ya Tehama pamoja na utafutaji wa masoko na kusema sekta hiyo inaenda kupata suluhu ya changamoto hizo.

Pamoja na hayo amesema njia ya kuondokana na changamoto hizo nikuwa na wawekezaji mahiri kama alivyo DP World.

Amesema katika ukanda wa Afrika yapo masoko yanayoshindaniwa likiwemo soko la Zambia,Malawi,Lwanda,Uganda pamoja na DRC ambapo inaelezwa kuwa mshindani mkubwa ni bandari ya mombasayenye gati 19 wakati bandari ya Dar se salaam ikiwa na gati 12.

Amesema bandari zote hasa kwenye maeneo yenye kontena zinahudumiwa na sekta binafsi na kulinganisha bandari ya Angila,Egipti,Gana na Nigeria kutokana na kuwa na uwezo mkbwa wa kufanya kazi kwa ufanisi.

“Tuliamua kuleta privacy sekta ambaye anauwezo wa kufikia viwango vya kimataifa pamoja na awe na ufanisi katika utekelezaji wa bandari ya Dar es salaam sifa ya pili ambayo privacy sector ambaye tunataka tumlete awe na uwezo wa kutoa ufumbuzi katika mnyororo mzima wa usafirishaji sifa ya tatu awe na mtandao mpana wakupata mizigo kutoka soko la usafirishaji Duniani na sifa ya nne awe na uwezo wa kimataifa katika kuendeleza na kuendesha shughuli za kibandari

Amesema Kampuni ya DP World inauwezo mkubwa katika uendeshaji wa shughuli za bandari Duniani kuanzia Afrika,Uraya,Marekani na kaskazini pamoja na kusinipamoja uzoefu wa kuchagiza nyororo mzima wa wa usafirishaji kutoka katika maeneo mbalimbali yanayozalisha bidhaa.

Pia amesema Kampuni hiyo inamiriki kampuni kubwa ya meri yenye takribani meli 100 ambazo zinafanya kazi za kibiashara duniani kote na kusema kampuni hiyo inaendesha maeneo mengi maalumu ya kiuchumi.

Amesema baada ya kumleta DP World yapo manufaa yatakayo patikana ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa Meli kukaa nangani,kupunguza muda wa ushushaji wa makontena kutoka siku nne mpaka kufikia siku moja na nusu,kuongeza mzigo kutoka tani Milioni 20.8 mpaka kufikia tani Milioni 47.57 ifikapo mwaka 2023/2033,kuongeza mapato yatakayotoka na kodi ya forodha ambapo kwa sasa Serikali inakusanya Tirioni 7.756 kupitia TRA. 

 

Previous Post Next Post