KWA HALI ISIYO YAKAWAIDA MTOTO ALIWA NA NGURUWE SUMBAWANGA

 

Na Fedrick Mbaruku 

MTOTO aliyefahamika kwa jina la Haruni Mwanakatwe (10) ambaye pia ni mlemavu mkazi wa mtaa wa Edeni B Kata ya Sumbawanga asilia Mkoani Rukwa ameuawa kwa kuliwa na nguluwe aliyekuwa na watoto wake nyumbani kwao.

Tukio hilo limetokea juni 25 mwaka huu majira ya saa 12:40 na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Mtaa Bw.Justine Daud,Simon Elias,pamoja na majirani wa mtaa huo.

Kwa mjibu wa taarifa za tukio hilo inaelezwa Mama wa Haruna alienda kanisani na watoto wengine wakati baba wa Mtoto Haruna alikuwa safarini na baada ya mama mzazi kurudi nyumbani alimkuta Haruna amejeruhiwa sehemu ya kiuno kwa kuliwa na nguruwe huyo.

Hata hivyo mtoto huyo alishindwa kuamka kwenda kujisaidia kutokana na tatizo la ulemavu wake na kupelekea kujisaidia sehemu alipokuwa amekaa na baada ya hapo mnyama nguluwe na watoto wake alienda kusukuma mlango mara baada ya kusikia harufu ya uchafu wa mtoto allipomaliza kula uchafu akamtafuna mtoto.

Mtoto huyo alikoswa uangalizi baada ya wazazi wake na ndugu zake kutokuwepo nyumbani ,pia ni kutokana na wakazi wa maeneo hayo kuwa na mifugo aina ya nguluwe wengine majumbani kwao .na hii inapelekea kutokuwa na umakini wa mifugo yao ikifikia kipindi cha wanyama awo wakati huowakiwa na watoto wanaweza kumla mtoto mdogo kwani unakuta wananjaa sana kwa kipindi hicho.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoani humo limewataka Wananchi kuondokana na Mila potofu na kuondoa hofu juu ya tukio hilo huku likiwataka kutoa taarifa mapema pale matukio mabaya yanapokuwa yametokea.

Previous Post Next Post