Na Fedrick Mbaruku
Mchezaji wa Club ya Yanga FC ambaye ni raia wa Ghana Bernard Morrison ameagana rasmi na Club hiyo hii leo 21 juni 2023 mara baada ya kuhudumu kwa muda wa misimu miwili.
Morriso awali baada ya kuto Ghana alisajiriwa na Club ya Simba SC au Wekundu wa Msimbazi na baada ya kuchezea timu hiyo kwa nyakati tofauti alisajiriwa na Club ya Yanga.
Inaelezwa kuwa hadi sasa Club ya Yanga imeachana na wachezaji watatu akiwemo Bernard Morrison,Tuisila Kisinda,Dickson Ambundo pamoja na Makocha wawili akiwemo Nessrendine.
Tags
MICHEZO