MWENYEKITI Wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dodoma Bw.Salum Shaban Salum amelitaka tawi jipya la umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) la Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Dodoma kuendeleza,kudumisha uzalendo pamoja na kuisemea Serikali kwa kazi zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.
Salum aliyasema hayo Mei 31,23023 wakati wa uzinduzi
wa tawi jipya la umoja wa vijana (UVCCM) ambapo alisema matarajio ya kufungua
tawi hilo ni kuongeza nguvu ndani ya Chama cha hicho pamoja na kuwaandaa vijana
kuwa wazalendo wa nchi ili kulinda amani,kuyasema yanayofanywa na serikali ya
Jamuhuri ya Muungano.
Pia Salum aliyabainisha mafanikio yaliyofanywa na
Serikali ya awamu ya sita hasa katika utekelezaji wa miundombinu mbalimbali
hususani katika sekta ya Elimu,Barabara,Maji sanjali na hayo ameitaja
miundombinu ya standard Gage,Uwanja wa Ndege wa kimataifa uliopo Jijini Dodoma
na ukamilishaji wa majengo mbalimbali ya serikali.
Nae Katibu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Dodoma Mjini
Makao Makuu ya Serikali na Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi Bw.Issack Ngongi
alisema kufuatia ufunguzi huo UVCCM watahakikisha wanaongeza wanachama ili
kuwezasha kufanya shughuli za Chama na kuisaidia katika kuleta maendeleo.
Alisema wanachama hao wapya wanatakiwa kuja kujiunga
na Chama hicho ni uzalendo huku akisema sera ya Chama cha Umoja wa Vijana wa
CCM ni ujamaa na kujitegemea.
“Leo tumefungua tawi hili la Chuo cha Uandishi wa
Habari na Utangazaji Dodoma kwahiyo tuhakikishe tunakuwa wamoja katika Wilayah
ii ya Dodoma Mjini lakini kushirikiana na Seneti ya Mkoa kwa kushiriki katika
shughuli za Chama na Serikali,”alisema