Taasisi ya Chama cha wanawake Jijini Dodoma (WAUVI) inatarajia kuanzisha Tuzo ya Mavunde ya wajasiliamali itakayolenga kupata kikundi cha kuongeza thamani ya mazao na mifugo kitakacho pewa mitambo na mashine yenye thamani ya shilingi 20,000,000.
Hayo yalisemwa Mei
30,2023 na Naibu Waziri wa kilimo na Mbunge wa wa Jimbo la Dodoma mjini
Mhe.Anthony Mavunde katika viunga vya Nyerere Squer Jijini Dodoma alipokuwa
akifunga mafunzo ya wajasiliamali Mkoa wa Dodoma.
“Niwapongeze sana
wanawake wa Dodoma na Chama kwa ujumla endeleeni kutoa elimu kuhusiana na
ujasiliamali ili kuweza kutibu suala la umasikini katika jamii zetu tuwajibike
kila mtu kwa nafasi yake bila kusahau malezi ya watoto wetu,”alisema
Nae Mwenyekiti wa Chama
cha Wanawake (WAUVI) Mkoa wa Dodoma Bi.Ester Said amesema lengo la Taasisi ya (WAUVI)
ni kukuza Viwanda vidogovidogo,kupanua wigo wa kibiashara na masoko,kutoa
mafunzo ya kielimu katika masuala ya kijamii,kitamaduni na kiafya,kuongeza
kipato kwa mtu mmoja mmoja na maarifa kwa ujmla katika nyanja tofauti.
Alisema katika Taasisi
ya (WAUVI) inatarajia kupunguza umaskini katika kaya maskini kwa
wanawake,kupunguza wimbi la watoto wa mitaani huku ikiahidi kuwapa kipaumbele
wanawake na watoto.
Pia aliwataka wanawake
kuwasaidia waume zao shughuli mbalimbali ili kuondoa sintofahamu zinazojitokeza
mara kwa mara ndani ya ndoa na badala yake kudumisha mahusiano ya kujenga jamii
bora.
“Kwetu sisi fursa hii
ujio wake umetupa faraja na matumaini makubwa pia tunatoa pongezi kwa wadu wote
walioshiriki kwa wakati wote wa program hii ya Zunguka na Mama Samia.
“Ushirikii wao umekuwa
chachu kwa ufanisi kwa program yote iliyotolewa kwa wajasiliamali wetu ni
matumaini yetu kuwa wataendelea kuwa nasi ili kuendeleza miongozo muhimu kwa
wajasiliamali wetu ili sote kwa pamoja tufikie ndoto ya kushiriki vyema uchumi
wa Viwanda,”alisema
Hata hivyo Said alisema
Taasisi hiyo imejipanga kusaidia serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuende
na kasi ya kupunguza ukosefu wa ajira nchini.
Alisema Taasisi hiyo
imekuwa na idadi kubwa ya usindikaji wa bidhaa mbalimbali ndani ya Mkoa wa
Dodoma na maeneo mengine huku akisema kuwa watu wameanza kupata mafunzo
mbalimbali ya kuendesha shughuli zao za kibiashara nchini.
Aidha Said alisema
Chama hicho hadi sasa kinawanachama takribani 3200 wanawake wakati idadi ya
wanaume ikiwa ni 500 na kusema Taasisi hiyo halhijabagua jinsia kwa lengo la
kuleta ushindani katika baadhi na kukuza soko la wajasilisiamali nchini.