Na Adolf Siwale
Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia wanawake na makundi maalumu Mhe.Dorothi Gwajima ameimba serikali kupitia wizara ya fedha kuelekeza bajeti kuu ya serikali katika kuimalisha usawa wa kijinsia nchini.
Waziri Gwajima ameyasema hayo Juni 13 mwaka huu aliposhiriki katika semina maalumu ya wabunge walipokuwa wakijadili mchakato wabajeti kuu ya Serikali kupitia Wizara ya fedha katika ukumbi wa Morena uliopo Jijini Dodoma.
Waziri Gwajima alisema kupitia bajeti hiyo serikali inatakiwa kuelekeza nguvu kwa wafanyabiashara wadogo kwani asilimi kubwa ya makusanyo ya pato la taifa linatokana na wafanya biashara wadogowadogo.
Gwajima alisema ili kumarisha maendeleo ya nchini lazima jinsia zote mbili zikae kwa usawa kwani kutokuwepo kwa usawa kati ya hizo jinsia mbili kunasababisha shughuli nyingi za kimaendeleo kukwama.
“Nimshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuunda wizara hii na kubwa zaidi rais naye ni kinara wa masuala ya jinsia katika maendeleo ya kijinsia.
‘’Na sio tu kinara hapa nchini ni mpaka dunia nzima na wakumuwezesha ili aendelee vizuri ni sisi wenyewe kama wizara hata katika bajeti yetu katika kifungu namba 118 utaona tumesema serikali tunazingatia misingi ya jinsia sera na bajeti ya serikali’’alisema.
Alisema wizara kwa kushirikiana na ofisi ya Mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) wameandaa nyaraka zitakazo saidia kusukuma uingizaji wa masuala ya kijinsia kuanzia mwakani na kuona kama kutakuwa na uwezekano wa sekta hiyo kutengeneza uwiano katika muelekeo wa kijinsia.
Naye mchambuzi na mtafiti wa masuala ya sera na kanuni za kibunge Mh. Deus Kibamba alisema bunge linaendelea na mchakato wa bajeti ili kupenyeza swala la kijinsia katika bajeti hiyo.
Kabamba alisema TGNP pamoja na taasisi mbalimbali nchini zinafanya utafiti na uchambuzi wa bajeti inayotarajiwa kuwasilishwa tarehe 15 Juni mwaka huu ili kuboresha maisha ya watanzania ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi.
“Mazungumzo hayo yalikuwa yanahusu jinsi waheshimiwa wabunge wanavyoweza kuboresha uwezo wao wa kuchangia bajeti.
“Wananchi wengi wamekuwa wakipenda wabunge waweze kuchangia kwenye mchakato wa bajeti, kutunga sheria kwahiyo leo tumeangalia kuwa wabunge wanawezaje kuongeza umadhubuti wao katika kupenyeza bajeti kwa mlengo wa kijinsia,” alisema.
Hata hivyo wabunge walisema kuna umuhimu wa wabunge kuwa na nafasi zao katika kutoa mchango wao ili halimashauri wanazozihudumia ziweze kupenyesha maswala ya kijinsia kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Walisema wanawake wanatakiwa kuchagizwa na kuhamasishwa katika kuingia kwenye nafasi za uongozi ili kuleta usawa wa kijinsia na kuongeza kuwa asilimia 97 ya wanaoshika nafasi katika uongozi ni wanume huku wakilingaisha na asilimia 3 ya wanawake.
“sisi kama wabunge na wawakilishi wa wananchi ni lazima tuwafikirie watu tunaowaonggoza hususan ni wanawake zaidi kwani mahitaji ya wanawake ni makubwa zaidi,” alisema Khadija Shaabani Taya mbunge wa viti maalumu.