YANGA MOTO HATUA YA FAINALI SHIRIKISHO BARANI AFRIKA(CAF)


 


TIMU ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya shirikisho barani Afrika (CAF) dhidhi ya Marumo Gallant yenye makazi yake Afrika Kusini na mtanange huo ulipigwa katika dimba la royal Bof Keng.

Mchezo huo uliwapa kibali wanajangwani kushiriki hatua ya fainali ambapo watakutana na Usm Alger ya Algeria timu hiyo imekuwa na mwendelezo mzuri wakutopoteza  michezo yake kuanzia awali mchezo wakwanza walicheza na timu ya Marumo wakiwa nyumbani walishinda mabao 2-0  na ugenini walishindamabao 2-1 wameweza kumaliza michezo yao wakiwa na mabao 3 ya faida na bao 1.

Timu hiyo kwa Mara ya kwanza imeweza kufuzu hatua ya fainali wakiliwakisha  taifa lao na kuipepelulusha bendera ya nchi yao kwa kishindo kikubwa.

"Sisi mashabiki tuna ahidi kuwapa ushirikiano kwanamna yeyote na tunawatakia maandalizi mema na kila la kher katika mchezo wenu wa fainali dhidi ya Usm Alger tuna amini kombe La shirikisho ni lakwetu tuna waamini wawakilishi wetu"walisema

Fiston Mayele pamoja na kenedy msonda walikatisha malengo ya timu ya Marumo Gallant baada ya kuwafunga mabao mawili yaliyowafanya alama za kushiri hatua hiyo kuishia njiani.

Licha ya vijana wa Marumo kuonyesha ubora wao na mashambulizi makali katika mchezo wao wa nusu fali wakutafuta alama za kuvuka hatua ya nusu fainali kwenda kwenye fainali  lakini juhudi zao ziligonga mwamba mbele ya wanajangwani alimaarufu kama wananchi.

 

 

 






Previous Post Next Post