Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Ikulu ya Chamwino iliyopo Jijini Dododma ambapo amesema kukamilika kwa jengo la Ikulu mpya ya ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa kwa ushirikiano kati ya ofisi ya Ikulu,Wakala wa majengo Tanzania (TBA) na shirika la uzalishaji mali na Jeshi la kujenga Taifa (JKT).
Dk.Samia ameyasema hayo leo 20 Mei 2023 alipokuwa akizindua jengo mpya la Ikulu ya Chamwino iliyoko Jijini Dodooma akiambatana na viongozi wengine wa serikali akiwepo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi,Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philp Mpango,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa,Marais wastaafu na Viongozi wengine.
Rais Samia amesema historia ya ujenzi wa Ikulu hiyo ni alama na uthibisho rasmi wa kukamilika kwa adhima ya serikali ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia amesema kufuatia ujenzi wa majengo ya serikali yaliyopo Msalato Jijini Dodoma katika ujenzi wa makao makuu watafika pia wageni wa mataifa mengine kisha kupokelewa kama ilivyo katika Ikulu ya Dar es salaam.
a mwenendo wa sasa upendo,maelewano na mshikamano ili kusaidia kuendeleza Taifa huku akisema waasisi wa taifa waliweka misingi imala ambayo itaendlea kudumishwa na kuimalishwa/
Dk.Mwinyi amesema ameishukuru serikali kwa kuipatia serikali ya Zanzibar sehemu itakayotumika kujenga Ofisi za Serikali hiyo ili kuwawezesha watumishi kupata mazingira bora ya utendaji kazi.
Pia Dk.Mwinyi amesema katika Ikulu mpya imetengwa Ofisi ya Rais wa Zanzibar huku akiipongeza serikali kwa hatua hiyo pamoja na wote walioshiriki katika ujenzi wa Ikulu hiyo likiwemo Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mawakala wa majengo Tanzania na kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.
Pamoja na hayo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philp Mpango amesema Ikulu hiyo imejengwa kwa nguvu zilizotokana na kodi za Watanzania huku akitoa maagizo kwa viongozi wa Ikulu kuliheshimu jengo hilo pamoja na kulitunza ili liweze kutoa maamzi sahihi na kumusaidia Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan katikati akiteta jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyeki wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussei Ali Mwinyi na Makamu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philp Isidor Mpango mala baada ya kukamilisha zoezi la uzinduzi wa Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.