Serikali imejipanga kuweka mipango mikakati ya kuanzisha Taasisi itakayo shughulika na masuala ya anga ikiwemo setilaiti ili kuakikisha matangazo yanarushwa nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Samia Suluhu Hassan leo mei 18 mwaka huu wakati apokuwa akizindua mnala wa Digital Television (DTT) Jijini Dar es salaam.
Dk.Samia ameipongeza kampuni ya Azam kwa kile alichokiita uwajibikaji bora wa maendeleo kutokana na kazi zinazofanywa na kampuni hiyo hususani katika kurusha matangazo yenye maudhui yanayoifunsha jamii pamoja na kuendelea kuitaarifu jamii kwa kila linaloendelea hapa nchini.
Dk.Samia amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi katika kuhakikisha uendelevu wa sekta ya habari na teknolojia na utangazaziji hazipati changamoto na kuipongeza wizara ya habari kwa hatua ilizozifanya mwaka 2021 hasa katika kufanya mapitio ya mfumo wa leseni zinazoziwezesha sekta ndogo kuboresha mazingira ya utendaji kazi katika sekta hiyo.
Pamoja na Rais Samia amesema yapo mambo mengi yanayohitajika ili kuendelea kufannya maboresho zaidi katika sekta ya habari nchini.
Katika hatua nyingine Dk.Samia ametoa wito kwa wadau wa habari nchi kuongeza jitihada ili kuivusha nchi nakuifikisha katika malengo tarajiwa katika sekta ya habari.
Amesema sekta hiyo ni muhimu katika masuala ya kimaendeleo ndani ya taifa huku akiielekeza wizara ya habari kuchukua hatua zote na kuwataka wadau hao kuyafanyia kazi maagizo hayo kwa kushirikiana na wadau husika ili kuhakikisha utendaji kazi wao unafanywa kwa uweredi na ufanisi.
Dk.Samia amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto katika sekta hiyo serikali na mamlaka husika zitahakikisha changamoto hizo zinataatuliwa kwa hali ya juu.
"Niwapongeze sana Azam Media Group kwa kuwekeza katika sekta ya sanaa mnatufunza kwakweli na tumekuwa kisawasawa ingawa bado tunaomba ladhi msituchoke muendelee kutushika mkono ili wanamichezo wetu na wasanii waendelee kukua zaidi na zaidi,"Dk.Samia