WIZARA YA ARDHI YAJA NA MBINU MADHUBUTI KATI YA SMT NA SMZ

 


Wizara ya aridhi nyumba na maendeleo ya makazi Tanzania bara na Visiwani Zanzibar pamoja na taasisi za shirika la nyumba za Taifa (NHC) na lile la Zanzibar (ZHC) zimesaini hati ya makubaliano katika sekta ya aridhi na Nyumba.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo 20 Mei mwka huu  ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa mwongozo wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Ofisi ya Makamu wa pili wa SMZ kuhusu Taasisi zisizo kuwa za Muungano kukutana na kubadilishanau nazo katika utendaji kazi huku Wizara hiyo ikijadili namna ya kukabiliana changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Zoezi la utiaji saini hiyo limeongozwa na Waziri wa aridhi Nyumba na maendeleo ya makazi Dk.Angelina Mabula na kufanywa na Katibu Mkuu Wizara ya aridhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi bara AnthonySanga na Mzee Miraji huku shirika la Nyumba la Taifa likiwakilishwa na Mkurugenzi wake Hamad Abdalah mbele ya Mawaziri wa sekta hiyo.


Dk.Mabula amesema makubaliano yaliyofanyika yaingie katika utekelezaji na yatoe fursa kwa kila mmoja kuona namna ya kuboresha mahusiano katika sekta ya aridhi na kueleza kuwa Tanzania bara sekta hiyo ni wezeshi na inapofanya vibaya inazikwaza sekta nyingine.

#mapinduzidigital#mapinduziupdates#mapinduzimedia#wizara_ya_ardhi

Previous Post Next Post