Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu Dk.Doroth Gwajima ametoa wito kwa wazazi na viongozi wa dini kote nchini kuhakikisha wanatoa elimu kwa watoto juu ya suala la malezi na makuzi ya familia ili kujenga jamii bora na yenye kuleta tija kwa taifa.
Waziri Gwajima ameyasema hayo leo mei 15 mwaka huu katika kilele cha maadhimisho ya siku ya familia duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika viunga vya Nyerere Squer Jijini Dodoma.
Waziri Gwajima amesema wazazi na walezi wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanayalinda maadili ya watoto katika kutoa elimu juu ya vitendo vya ukatili vinavyoendelea hapa nchini.
Ameseama mmomonyoko wa maadili umechangiwa na utandawazi ikiwa ni pamoja na matumizi hasi ya mitandao ya kijamii huku aiiasa jamii kutafuta matumizi sahihi ya mitandao ili kuzinusuru familia dhidi ya vitendo vya kikatili.
Kwa mujibu wa takwimu inaelezwa kuwa mwaka 2021/2022.Mwaka 2021 zaidi ya watoto 11,469 wakati takwimu za mwaka 2022. 12,168 wakati walitakiwa 6335 kuwalawiti ni 1555 mwaka 2021 walikuwa 1124 huku akibainisha kwa 60% ya wazazi au walezi humalizana wao kwa wao majumbani mwao.
DK. Gwajima ameainisha mikoa anayo ongoza ikiwemo Mkoa wa Arusha ikiwa na idadi ya vitendo vya kikatili 28,0000 Mbeya 610 Mwanza 795 kinondoni 681 Tanga 905 huku akiwataka wazazi kuacha kufumbia macho vitendo hivyo badala yake walio patwa na matatizo haya kupatiwa msaada zaidi.
Pia amesema vitu vinavyo changia hasa suala la mmomonyoko wa maadili ni Mira, desturi,Tamaduni na maswala ya kuiga ambavyo chanzo chake kikitajwa kuwa ni utandawazi wakati huku akiiasa jamii kutafuta sehemu nzuri ya utandawazi hali ambayo itapunguza kiasi cha mmomonyoko wa maadili.
Aidha katika hatua nyingine Waziri Gwajima amezindua kampeni ya kitaifa ya elimu ya mmomonyoko wa maadili ambayo kitaifa yatafanyika ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi juni mwaka huu na hatua ya kwanza ikiwa ni utekelezaji wa kaulimbiu"Maadili yetu Taifa letu".
"ninaimani kongamano hili litatoa fursa kwa wazazi na walezi kutoa aina ya malezi yaliyobora na ya kufaa kwa watoto wetu ili kuenenda na wakati wa sasa tusiwasahau watoto wala tusijikite bize familia kwanza wazazi tuwe mstari wa mbele kukemea vitendo vya ukatili hasa watoto kulawitiwa,kubakwa na vingine vingi,"waziri Gwajima
Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu Dk.Doroth Gwajima katikati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamle kulia wakiwa katika picha ya pamoja katika kilele cha maadhimisho ya siku ya familia duniani.