JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LAANZA KUWASAKA WANAOWALAZIMISHA WATU KUFUNGA BIASHARA KARIAKOO


 Kufatia sakata la kutofungua na kufungwa kwa Maduka ya Wafanyabiashara Kariakoo Jijini  Dar es salaam Kamanda wa Jeshi Kanda maalumu ya Dar es salaam Jumanne Murilo amesema jeshi linafanya Opalesheni ya kutafuta kikundi cha kuwalazimisha watu kutokufanya biashara.

Murilo ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam alipotembelea katika maeneo ya Soko la Kariakoo kulikozuka sintofahamu ya kufungwa kwa maduka mala baada ya kuzuka taarifa za uwepo wa kikundi cha watu wanaopita katika maeneo mbalimbali wakiwalazimisha watu kufunga shughuli zao za biashara.

Amesema Wafanyabiashara wanatakiwa kuendelea na shughuli zao pasipovitisho vya aina yoyote "Suala la kufunga au kutofungua ni suala binafsi kwa hiyo kama kuna watu wanataka kufunga maduka yao wafungue hawapaswi kutishwa kwa vyovyote vile" Murilo

"Kila mtu ana uhuru wa kufanya anachotaka kukifanya kwa hiyo sisi tumekuja kuangalia kama kuna kikundi kinapita kulazimisha wasifanye biashara hicho ndicho tunakitaka na itakuwa ni halali yetu na inabidi tukionye kwa kina"

Kamanda Murilo amewatayarisha wananchi Mkoani humo juu ya suala la kuingilia uhuru wa mtu katika shughuli ya biashara.

 

Previous Post Next Post